ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, February 28, 2014

SIMBA; TUTAIDUWAZA RUVU SHOOTING ILI HESHIMA YETU IRUDI

Kikosi kilichokosa muelekeo wa kutwaa ubingwa wa Tanzania bara timu ya Simba Sc ,kimeapa kuwa lazima izipate alama zote tatu katika mechi inayofuata dhidi ya Ruvu Shooting.

Wakiongea na blog ya Simba Platinum Supporters mshambuliaji wa kimataifa wa burundi Amissi Tambwe na beki ya kati Donald Musoti, wamesema kuwa wanafahamu kuwa wanachama na mashabiki wa Simba wamekata tamaa na timu yao lakini hilo lisiwavunje moyo kwani timu iko katika hali nzuri na watacheza vizuri zaidi ili kuweza kuondoka na alama zote.

Simba iliyo katika kiwango kisichoridhisha ,inahitaji ushindi wa aina yoyote ile ili kuweza kujipalilia nafasi nzuri zaidi itakayoifanya iweze kushiriki michuano ya Afrika mwakani.

Wakati huo huo, mchezo utakaofanyika jumapili dhidi ya Ruvu Shooting,huenda ukashuhudia urejeo wa Captain Massoud Nassor Chollo baada ya afya ya mchezaji huyo kuimarika.

NI REKODI TU NDIYO INAYOIBEBA AL AHLY DHIDI YA YANGA HAPO KESHO

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Dar Young Africans, kesho kinajitupa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuwavaa Mabingwa watetezi wa Afrika National Al Ahly.

Katika mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu hiyo, Yanga itaingia dimbani huku ikiongozwa na nyota wa kimataifa mwenye uchu wa magoli Emanuel Arnold Okwi.
Ikumbukwe kuwa katika mechi sita ambazo Yanga imefanikiwa kucheza dhidi ya AL Ahly haikuwahi kushinda mchezo wowote zaidi ya kutoa sare katika michezo miwili.

Yanga iliyo katika kiwango cha hali ya juu hivi sasa,inahitaji ushindi wa aina yoyote dhidi ya miamba hiyo ya Afrika ili kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu raundi ya pili ya michuano hiyo.

Wednesday, February 26, 2014

UKOSEFU WA FIKRA CHANYA WA BAADHI YA WANACHAMA WA SIMBA SC,HUKUMU YAKE NDIO HII

Takriban mwaka wa pili sasa, mashabiki wa Simba wanaendelea kuangalia muenendo mbovu wa timu yao.
Mashabiki pamoja na wanachama wengi wao wanawalaumu wachezaji kuwa wao ndio haswa kiini cha timu kufanya vibaya,wanawadhihaki,wanawatukana na kuwaambia kila aina ya neno baya na hata wengine kufikia hatua ya kutaka kuwapiga wachezaji wao bila kujua nini tatizo.

Siwezi kuwalaumu sana ila nachowalaumu ni kitu kimoja tu,kwanini wanatoa hukumu pasipokuwa na hakika??
Kumlaumu mchezaji kuwa anaihujumu timu pasipokujua anaishi vipi au kipi anakosa ni dhambi ambayo ikiendelea itatuhukumu,ingawa Simba ina bahati ya kupata wachezaji wanaoienda timu yao,mwisho wa siku na wao watachoka tu.

Tatizo kubwa la Simba SC walilianzisha wanachama wa timu hii. Wanachama hawa pasiokuelewa au pasipokufahamu wakakubali kuingia mikononi mwa mwenyekiti ambaye afahamu majukumu yake ndani ya Simba SC BW Ismail Aden Rage.

Yawezekana labda ni kwa sababu ana majukumu mengi lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rage ndiye kiini cha tattizo.

Rage ilipaswa afahamu matatizo ya timu yake na sio kuja na hoja nyepesi eti kuwa yeye hachezi pale timu inapofanya vibaya., Ikumbukwe kuwa maandalizi ya mpira wa miguu popote pale duniani yaanaanzia nje na ndani ni utekelezaji tu.

Lakini wanachama hawalioni hili wao wanawalamikia wachezaji peke yao.

KAMATI YA UTENDAJI
Wengi ya wanachama hawafahamu hii kitu, binafsi naweza kusema hapa ndipo kila kitu kwa Simba SC,.
Siku chache zilizopita kamati yetu ya utendaji iliamuru kumpiga chini Rage ili angalau timu yetu ikae sawa,ni kweli lilikuwa wazo zuri ila tatizo njiac waliyopitia ilikuwa dhaifu.

Rage aliporudi alidai kuwa hatambui mapinduzi hayo, Kamati ikawa imetulia kana kwamba haijui nini cha kufanya wakati katiba ya Simba iko wazi.

Katiba inasema wazi kabisa kuwa kama wajumbe wa kamati ya utendaji watajiuzuru,basi automatically Mwenyekiti naye anapoteza hadhi ya kuwa kiongozi. wajumbe hawakufanya hili matokeo yake ni wapo kama hawapo.

Hii ni mbaya sana, ni wajibu wanachama kufahamu tuhuma za kwanza wapeleke kwa viongozi wao na si wachezaji wa Simba peke yao. Sana sana mnavunja ari yao tu ya kujiamini pindi pale wanapokuwa uwanjani na nyinyi mkiwa mnaangalia.

TUKUBALI TULIKOSEA KUCHAGUA,ACHA TUHUKUMIWE KWA DHAMBI ZA KUCHAGUA KIBAYA KATIKA TIMU YETI!

TWAHA MAJERUHI YAANZA UPYA

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba SC ya mitaa ya Msimbazi Ibrahim Twaha Shekua maarufu kama Neymar wa msimbazi,anapitia katika kipindi kingine kigumu katika maisha yake ya soka baada ya kurejea tena maumivu katika eneo la paja katika mguu wake.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa na hamu ya kurudi uwanjani ili kumthibitishia kocha wa sasa wa Simba Zdravko alugarusic kuwa yuko sawa,inabidi aongezewe wiki zaidi kabla ya kurejea tena uwanjani.
Ikumbukwe kuwa Twaha aliumia katika mazoezi ya kujiandaa na pambano la Yanga lililoisha kwa sare ya 3-3.

Hili litakuwa pigo lingine ambalo linaifanya klabu hiyo kuanza upya baada ya juzi kumpoteza mshambuliaji Zahoro Pazi ambaye naye kwa sasa ni majeruhi .

Tuesday, February 25, 2014

ZAHORO APATA MAJERAHA MAZOEZINI LEO HII, HENRY SAFIIIIIIIIII

Mshambuliaji wa timu ya Simba SC Zahoro Pazi amepata maumivu makali baada ya kugongana na beki Haruna Shamte katika uwanja wa kinesi,.

Zahoro ameumia muda mfupi baada ya Simba kushuhudia urejeo wa makinda ya ajabu Abdallah Seseme na Ibrahim Twaha.

Ikumbukwe kuwa, Simba Sc itabaki kuwa na washambuliaji pekee wawili wa kutumainiwa ambao ni Amissi Tambwe na Bentram Mombeki.

BREAKING NEWSSSS, MAPUNDA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Goli kipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania na Simba SC amefiwa na baba yake mzazi leo hii.

habari kamili zitafuata.......

JE UWEPO WA DONALD MUSOTI ,NI MWISHO WA GILBERT KAZE SIMBA SC?


Sunday, February 23, 2014

SIMBA YAPIGWA TATU TAIFA

Timu ya Simba SC,leo imedhihirisha kuwa haina mpango wa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara,baada ya kukubali kichapo kitakatifu cha goli 3-2 kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu.


Ikicheza bila ya nyota wake Ramadhan Singano Messi,Simba ilicheza mpira dhaifu ambao ulikuwa hauna ufundi wowote.

Shukrani kwa mshambuliaji raia wa Burundi Amissi Tambwe kwa kufunga goli mbili leo hii!

YANGA WAJIPIGILIA MSUMARI WA MOTO BAADA YA KUMCHEZESHA OKWI

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Dar Young Afrika, wamejiweka katika wakati mgumu baada ya kumchezesha mchezaji mwenye utata wa usajili Emanuel Okwi katika mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.

Okwi ambaye alizuwa na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF,alicheza mchezo wa jana na kufunga goli safi kabisa katika kipindi cha kwanza.

Ikumbukwe kuwa, TFF iliomba muongozo FIFA kuhusu nyota huyo wa Uganda The Cranes, kabla ya FIFA kuiamuru TFF Ifuatilie umakini wa usajili wa mchezaji huyo ambapo TFF hawakufanya hivyo.

Yanga, jana iliweza kufanya kufuru ya soka baada ya kuiua timu iliyoonekana ngumu ya Ruvu Shooting kwa kipigo cha kihistoria cha goli 7-0.

TWAHA AANZA RASMI MAZOEZI KESHO,HUGO KITAAAMBO

Wachezaji wawili wenye kasi ya ajabu Ibrahim Twaha Shekuwa maarufu kama Neymar wa msimbazi pamoja na Abdallah Seseme Hugo wanarejea rasmi kikazi zaidi baada ya kuwa nje ya uwanja takriban miezi mitatu.

Twaha ambaye alipata maumivu ya paja baada ya kuanguka vibaya kwenye mazoezi ambapo Simba iliweka Camp ya muda kwenye uwanja wa Bamba Beach,anarejea kesho kikazi huku akiwa na hamu ya kumthibitishia kocha wa sasa wa Simba SC Zdravko Lugarusic kuwa yeye anastahili kuwemo kwenye kikosi cha kwanza.

Wakati IBRA akiwaza hayo,mwenzake Abdallah Seseme maarufu kama Hugo naye ameanza mazoezi tangu wiki iliyopita.

Ikumbukwe kuwa Hugo aliumia katika mazoezi katika uwanja wa kinesi jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo, Simba Sc leo inatarajiwa kumkosa Ramadhan Singano Messi na kushuhudia urejeo wa Edward Christopher katika kikosi kamili cha kwanza.

SIMBA KUWAVAA JKT RUVU LEO

Kikosi cha Simba SC,kinaingia katika mtihani mgumu leo hii pale itakapowakaribisha maafande wa JKT ruvu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ikitoka kulazimishwa sare na timu inayokuja kwa kwa kasi ya MBEYA CITY, Simba inahitaji ushindi tu ili iendelee kuwemo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.
Ikumbukwe timu hiyo inayosifika kwa soka la kasi na pasi fupi fupi,inaingia katika uwanja wa taifa huku ikiwakosa nyota wake Ramadhan Singano mwenye kadi tatu za njano na Harun Chanongo aliye majeruhi.

Sunday, February 9, 2014

HII YA MALINZI KIBOKO


Na Baraka Mbolembole
Mabepari wapo kila mahali, pia wana misingi mikubwa ya kifedha, na mahusiano makubwa na vyombo vya umma. Kwa mfano wana uhuru wa kutumia vyombo vya habari. Ila kama kiongozi anakuwa akiwavutia watu, basi ni kwa sababu ni kwa sababu yeye mwenyewe amavitiwa na hiyo kazi iliyo mbele yake. Watu ndiyo nguvu pekee inayoweza kusaidia mabadiliko. Hivyo kiongozi anatakiwa kuwaunganisha watu na kuwafahamisha kwamba umoja wao utasaidia kupata wanachotaka. Ila watu nao wanatakiwa kuamka.

Katika soka la Tanzania,  tunaweza kusema kuwa tumempata mtu ambaye tulikuwa tukimuhitaji, kwani  rais wa sasa wa Shirikisho la Soka Nchini, TFF, Ndugu, Jamal Malinzi  anaijua Jiografia ya Tanzania, na analifahamu vizuri soka la nchi hii.  Hivyo atakuwa anafahamu mahitaji  na mawazo yanayotakiwa ili kukuza mpira wa Tanzania. Malinzi licha ya kutajwa kama kiongozi hodari baada ya kupita kwa zaidi ya siku 100 za utawala wake, ameonesha kuwa muhubiri hodari shupavu, na bila shaka atakuwa mwanafunzi hodari pia. Na hili litawezekana endapo ataamua kutumia muda wake kutazama na kujifunza zaidi kuhusu nini hasa kinachotakiwa kuanza ili kupata msingi imara wa mpira wetu.

Soka mara zote linakuwa na mahitaji ya muda mfupi na muda mrefu. Malinzi ameingia na mipango yake, huku soka la vijana likiwa kipaumbele kikubwa kwake, na hapo Academy za soka anaamini ndiyo suluhisho la kwanza. SAwa ni jambo zuri kwa kuwa ameingia huku akiwa na kiu ya kufanikisha mipango aliyojiwekea. Sera yake kuhusu soka la vijana ni nzuri, na ziara yake aliyoifanya siku za nyuma katika Academy ya Allience Sports ya jijini Mwanza, ilirutubishwa na maneno mazuri kuwa hapo ndiyo kutakuwa kitovu cha mpira wa Tanzania. Hadi sasa Malinzi ameonesha kuwa mtu anayependa sana kazi yake, ila mikakati yake ni lazima iendane na uhimarishaji wa soka la mitaani.

Jiografia ya Tanzania, bado mchezo wa soka unahitaji unahitaji kuwekewa mkazo mkubwa sana katika ngazi za chini, kata, tarafa, wilaya na mikoani, kwa kuwa uchumi wetu hauwezi kuendana na mkakati wa Academy kwa nchi nzima. Vipaji ni vingi sana nchini. Labda huu ni wakati wa kuanzisha ligi za vijana ambazo muendelezo wake utakuwa hadi ngazi ya Kitaifa, kwa kuwa na michuano inayotambulika na si hii ya muda mfupi kama ilivyo Copa Coca Cola. Mfano michuano hiyo ya Copa, inaweza kufanyika kwa kipindi cha mwaka mzima kwa mtindo wa ligi. Ni ghali sana, ila udhamini ambao makampuni yanapewa katika soka la Tanzania unatakiwa kuendana na hali halisi. 

Mitaani, ndipo soka linapotoka. Ndiyo maana WAingereza wanataka kuhamia na kuweka nguvu zao zaidi katika soka la mitaani kuliko lile la mfumo wa Academy. Muundo mzuri wa mfumo wa soka uhusishe pia namna ya kuendeleza vipaji ambavyo kimsingi haviwezi kupata nafasi katika Academy kuwa kuwa mambo ya uchaguzi huendana na ukiritimba mkubwa kila mahali. Uzuri wa Academy ni kwamba vijana watakuzwa na kuendelezwa katika mwendo mzuri wa kinidhamu, kutambua majukumu na kuwajibika, ila siku zote ni lazima tutambue kuwa, kila mtoto huzaliwa na tabia njema, tabia mbaya huja baadae. UNaweza kuzalisha wachezaji 100 bora katika nchini na kujona umefanikiwa sana, ila tabia zao kadri wanavyokuwa wakikua zinakuwa zikibadilika. Soka la Academy ni muhimu, ila soka la mtaani ni tumaini la muda wote kwa mpira wa Tanzania.

Majuzi nilikuwa nikiwasiliana na James Julius,  Mtanzania ambaye yupo nchini Afrika Kusini, akifanya kazi katika Academy ya ' Stars of Africa'. Naye ameanza na mikakati ya kufanya uwekezaji katika soka. Ameomba ekali zaidi ya 20 katika mji wa Mwanza ili kuanza ujenzi wa ' Mandozi Sports Academy', maombi yake hayo anataraji kupata majibu mwezi huu. Huyu ni kijana mdogo tu na tayari ametumia zaidi ya millioni 20 kwa kuanzisha timu nne za vijana, U20, U17, U14, na U12. Mimi alinipatia CD za hiki ninachokisema hapa na nimeona mikakati yake. Hivyo kwa Malinzi, bila shaka tayari ametoa mwamko na matumaini kuwa watu wamemuelewa na tayari wanatumia nguvu zao kusaidia soka la Tanzania

Hapa ni makampuni yanayotakiwa kusaidia katika ili na si kusubiri kujitokeza hapo baadae wakati wakiona kuna matunda ya wao kutangaza biashara zao. Makampuni mengi yamekuwa yakijinifaisha kupitia ufadhili wao katika soka la Tanzania, Hata udhamini wanaoupata timu zetu mbili kubwa kwa sasa hauendani na thamani ya klabu hizo. Simba na Yanga zinawaingia faida kubwa wadhamini wao kuliko kile wanachoingiza wao kutokana na ufadhili au udhamini walionao. Makakati, wa Mandozi, Sports Acacemy, Allience Sports Academy unatakiwa kusapotiwa kwa nguvu na makampuni yaliyopo nchini. Yatafikaje, ni kwa wahusika wenyewe kujitokeza na kuonesha kuwa wapo tayari kufanya kitu kikubwa hivyo wanatakiwa kuyafuata makampuni hayo na kuyaomna yaende kuwasaidia.

  WANAOSEMA TFF IMEJAA, U- SIMBA NA U-YANGA NAWASHANGAA

Hivi ni nani anayeweza kuishi nje ya fikra za Simba na Yanga? Labda kwa yule ambaye si mpenzi wa soka. Wakati mwingine sisi binadamu tunakuwa wanafiki kweli. Nani hajui kuwa Jamali Malinzi amewahi kuwa kiongozi wa juu wa klabu ya Yanga? Nani hajui kuwa Geofrey Nyange Kaburu amewahi kuwa kiongozi wa juu wa klabu ya Simba> Vipi kwa kina Abbas Tarimba, Seif Ahmed, David Mosha, Zacharia Hans Poppe, Clement Sanga, mimi ninafikiri muhimu ni kuwashauri kuwa mpira wa Tanzania unawategemea sana wao hivyo wanatakiwa kufanya kazi zao kutokana kanuni na taratibu zilizopo. Wasiweke mapenzi ya vilabu vyao katika mambo muhimu.

Mimi, wewe, sote tumekuwa na upenzi wa soka. Inategemea tu, wewe utakuwa unaangukia wapi katika mapenzi yako, inaweza kuwa Simba, au Yanga ama timu nyingine yoyote ile. Ndiyo, Malinzi amewavuta watu wengi wa Simba na Yanga katika kamati zake, ila si kwa lengo la kuharibu mpira bali kupanga na kusimamia vuzuri mikakati inayoweza kusogeza soka la Tanzania mbele zaidi. Ni makosa kumuhukumu kwa sasa ila hatutosota kumsema vibaya endapo tunashuhudia kamati zake zikifanya mambo kwa kuvutana kisa mapenzi ya u- Simba na u- Yanga. Kwa sasa tuwasisitize wafanye kazi zao vizuri bila kusukumwa na ushabiki na si kuwahuku kwa makosa yasiyokuwepo. Kama hatuwataki hao, kisa ni Simba na Yanga, mleteni basi Sir Alex Ferguson aje kuwa rais wa TFF, kwa kuwa watu wengi wa soka wanatoka katika mapenzi ya dhati ya Simba na Yanga.

Itakuwa ni makosa makubwa kwa Malinzi, endapo watu aliowaamini na kuwapatia nafasi watamuangusha kisa ushabiki wa klabu zao. Itakuwa ni sawa na muwindaji ambaye aliamua kuchukua mtoto wa Simba na kumpeleka nyumbani kwake. Huyu atakuwa amejipelekea maangamizi yeye mwenyewe na familia yake. Soka la Tanzania halihitaji wafanyakazi wa mapenzi, ila ukweli ulio wazi linawahitaji watu waliopita Simba au Yanga, iwe kiuongozi au kiuchezaji. Mkakati wa Malinzi na soka la Tanzania unahitaji fikra zetu sote. Kulaumu kupo tu kila mahali, ila nasi tutoe ushauri mzuri kwao ili kwenda sambamba na matarajio yanayokusudiwa. Nimewasilisha tu. Karibuni pia Mandozi Sports Academy...

SIMBA 0-1 MGAMBO , MBEYA CITY 2-1 MTIBWA

Simba Leo imeambulia pat upi baada ya kufungwa goli 1-0, na Mgambo .

Wakati huo huo timu ya Mbeya City imeifurumsha Mtibwa kwa jumla ya goli 2-1

ORODHA YA WAJUMBE WA KAMATI MBALI MBALI ZA TFF


JUDICIAL ORGANS, INDEPENDENT & STANDING COMMITTEES TFF
BOARD OF TRUSTEE; Said Hamad El-Maamry, Stephen Mashishanga, Dr Ramadhan Dau, Joel Bendera, Mohamed Abdul Aziz
Kamati ya Nidhamu; Tarimba Abbas (Mwenyekiti), Advocate Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma, Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu; Profesa Mgongo Fimbo (Mwenyekiti), Advocate Hamidu Mbwezeleni (Makamu Mwenyekiti), Titus Bandawe, Twaha Mtengera, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Kamati ya Maadili; William Erio (Mwenyekiti), Advocate Ezekiel Maganja (Makamu Mwenyekiti), Advocate Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili; Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan Dyamwale.
Kamati ya Uchaguzi; Advocate Melchesedeck Lutema (Mwenyekiti), Advocate Walter Chipeta (Makamu Mwenyekiti), Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura, Hassan Dalali.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi; Advocate Julius Lugaziya (Mwenyekiti), Advocate Mwita Waissaka (Makamu Mwenyekiti), Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga, Masoud Issangu.
Kamati ya Fedha na Mipango; Wallace Karia (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammad, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy, Cyprian Kuhyava.
Kamati ya Mashindano; Geofrey Nyange (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald Ambi, Davis Mosha, Said George, Nassoro Idrissa (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Ufundi; Kidao Wilfred (Mwenyekiti), Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedastus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo, Dk. Cyprian Maro (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana; Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti), Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya, Ibrahim Masoud (Mshauri wa Ufundi wa Rais- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake; Lina Kessy (Mwenyekiti), Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amina Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o, Ingridy Kimaro.
Kamati ya Waamuzi; Saloum Umande Chama (Mwenyekiti), Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi, Zahra Mohamed.
Kamati ya Habari na Masoko; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela, Juma Pinto.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji; Advocate Richard Sinamtwa (Mwenyekiti), Advocate Moses Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko, Imani Madega.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha; Ramadhan Nassib (Mwenyekiti), Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga, Elias Mwanjala.
Kamati ya Tiba; Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema, Asha Sadick.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni; Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti), Shaffih Kajuna Dauda (Makamu Mwenyekiti), Boniface Pawasa, Deo Lucas, Juma Mgunda, John Kanakamfumu, John Mwansasu.
AD HOC COMMITTEES
Kamati ya Kutathimini Muundo wa Ligi; Dk. Mshindo Msolla (Mwenyekiti),Idd Mshangama (Katibu), Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir, Lucas Kisasa.

Kamati ya Kutathimini Muundo wa Bodi ya Ligi; David Nchimbi (Mwenyekiti), Edwin Kidifu, Jones Paul, Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani, Pelegrinius Rutayuga.

Friday, February 7, 2014

OKWI, CHUJI OUT YANGA KESHO



UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema hauna uwezo wa kumtumia mshambuliaji, Emmanuel Okwi, licha ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), kutoa leseni ya kucheza michuano ya klabu bingwa mwaka huu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema hadi jana walikuwa wakifuatilia kwenye mtandao wa CAF kuona iwapo kuna pingamizi lolote kwa mchezaji huyo.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani keshokutwa kumenyana na Komorozine de Domoni kutoka Comoro katika mechi ya awali ya michuano ya klabu bingwa Afrika itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kizuguto, alisema kwenye mfumo wa usajili wa Okwi, wamegundua hakuna dosari yoyote kwa vile walifuata taratibu zote, ikiwemo kuzungumza na mchezaji na kisha klabu ya Villa ya Uganda, ambayo imetoa ruhusa ya kusajiliwa kwa mchezaji huyo.

Hata hivyo, Kizuguto alisema wanaendelea kusubiri taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kama litatoa baraka zake kwa mchezaji huyo kuichezea Yanga katika michuano hiyo na ligi kuu msimu huu.

Okwi alisajiliwa na Yanga mwaka jana kutoka SC Villa baada ya kugoma kuendelea kuichezea Etoile du Sahel ya Tunisia, iliyomsajili kwa mkataba wa miaka minne kuanzia Januari mwaka juzi kutoka Simba SC ya Tanzania.

Nyota huyo wa Uganda, alifungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), akilalamika kutolipwa mishahara ya miezi mitatu na Etoile, ndipo akaruhusiwa kujiunga na SC Villa ya Uganda, ambayo baadae ilimuuza kwa Yanga.

Hata hivyo, baada ya Villa kumuuza Yanga ikidai ina haki zote, TFF imeandika barua FIFA kutaka ufafanuzi kama inaweza kumuidhinisha Mganda huyo kucheza timu ya Jangwani na wakati huo huo imeizuia klabu hiyo kumtumia hadi majibu yapatikane.

Hadi sasa Etoile haijailipa Simba SC dola za Marekani 300,000 za manunuzi ya mchezaji huyo na Wekundu hao wa Msimbazi nao wamefungua kesi FIFA.     

"Sheria inasema kabla ya kumsajili mchezaji inabidi mkubaliane, tulifanya hivyo na kisha tukazungumza na viongozi wa Villa na kisha tukatuma jina na mambo muhimu CAF, usajili wake umekamilika, kama kungekuwa na pingamizi tusingeweza kupata system na password," alisema Kizuguto.

Amesema baada ya kipindi cha pingamizi kupita, Okwi aliwekewa pingamizi baada ya siku 37 kwenye Shirikisho la Soka nchini, kitu ambacho nina imani CAF hawana taarifa nacho.

Kauli ya kiongozi huyo, imekuja siku chache baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, kusimamisha usajili wa mshambuliaji huyo Yanga hadi FIFA itakapotoa ufafanuzi.

Shirikisho hilo, limechukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Okwi, aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu cha miezi sita kutoka FIFA.

FIFA inazo kesi tatu mkononi za mchezaji huyo, ikiwemo ya kuishitaki Etoile  kwa kutomlipa mshahara wakati Etoile nayo imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. 
Simba nayo imeishitaki Etoile wa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000 (sh. milioni 480).

ATHUMAN IDD 'CHUJI'
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, amesema kiungo wao mahiri, Athuman Idd 'Chuji' ataukosa mchezo wa keshokutwa dhidi ya Wacomoro kutokana na kukabiliwa na adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo kati ya Yanga na Zamalek ya Misri.

Kizuguto alisema jana kuwa, wamepokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF), likiwakumbusha kuacha kumtumia nyota huyo kwenye mchezo huo kwa vile alipewa kadi nyekundu.

Yanga ilishiriki na kutolewa raundi ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa Afrika 
mwaka 2012 baada ya kufungwa na Zamalek ya Misri. Katika mechi ya kwanza,
walilazimishwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na katika mechi ya marudiano walifungwa bao 1 – 0 mjini  Cairo.

SEIF AHMED'MAGARI'
Mwenyekiti wa mashindano ya kimataifa wa klabu ya Yanga, Seif Ahmed 'Magari', amesema wana imani na kikosi chao dhidi ya Komorozine de Domoni.

Magari alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, tayari wameshagawa kazi kwa kamati yake, ambapo wakimaliza mchezo wa marudiano, watahakikisha wanaanza kuifuatilia timu ya Al Ahly ya Misri ili kujua mbinu zao zote.

Kiongozi huyo alisema wamejipanga kuweka historia barani Afrika mwaka huu kwa vile kikosi chao kimekamilika kila idara baada ya kufanya usajili kwa umakini mkubwa.

Ameongeza kuwa, lengo lao ni kuona Yanga inavuka vikwazo vya timu za Misri na kusonga mbele katika michuano hiyo.

"Tunajua wazi kwamba waarabu wanajua mbinu za kusaka ushindi nje ya mchezo, lakini tutatuma watu kufahamu mbinu zao na mahali ambapo Yanga ikienda Misri itafikia,"alisema.

WAAMUZI
Shirikisho la Soka Barani Afrika( CAF), limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi kati ya Yanga na Wacomoro itakayofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.

VIINGILIO
Uongozi wa Yanga umetangaza viingilio vya mechi ya klabu bingwa Afrika itakayoikutanisha Yanga na Comorozine de Domoni ya Comoro, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa sh. 5,000.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kiingilio cha juu katika mechi hiyo ni VIP A sh.30,000, VIP B na C Sh. 20,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 10,000 na viti vya kijani sh.5,000.

Alisema Klabu ya Yanga imetengeneza tiketi 45,000 ambapo katika VIP A kuna tiketi 500, VIP B na C tiketi 4,500, viti vya rangi ya chungwa tiketi 7,000 na viti vya kijani tiketi 33,000.

Alisema tiketi hizo, zitapatikana katika vituo 10 ikiwemo makao makuu ya klabu hiyo Jangwani, Olicom Buguruni, Stears, Oilcom Ubungo, Kimara Mwisho, Uwanja wa Uhuru, Shule ya Benjamin Mkapa pamoja na Uwanja wa Taifa.

AZAM KUWEKA REKODI



WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam watawakosa nyota wao wanne katika mechi ya awali dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbuji, itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Nyota wa Azam watakaokosekana katika mechi hiyo ni pamoja na mshambuliaji hatari, John Bocco na beki Hajji Nuhu, ambao ni majeruhi. Wengine ni chipukizi Ismail Lugambo na Farid Musa.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffari Iddi alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Bocco bado majeruhi wakati Nuhu aliumia goti juzi baada ya kuanguka ghafla wakati wa mazoezi yaliyofanyika Chamazi.

Jaffari alisema Lugambo alivunjika mguu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Azam na Ashanti wakati Farid amekuwa akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara na itabidi afanyiwe vipimo vikubwa.

"Farid itabidi afanyiwe vipimo vya MRY kwenye mgongo ili tujue sababu ya kuumia mara kwa mara na Bocco bado goti lake halijawa sawa. Alipewa mapumziko ya wiki mbili na tayari ameshamaliza wiki moja, hivyo hatacheza mchezo huo," alisema Jaffari.

Pamoja na kuwakosa nyota hao, Jaffari alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Ferroviario na kusisitiza kuwa, wamepania kuweka rekodi ya kufika mbali zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka jana.

Aliongeza kuwa, wamefurahi kupata ruhusa kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya kucheza mechi hiyo kwenye uwanja wa Chamazi kwa vile wachezaji wao wameuzoea na watautumia vizuri kupata ushindi.

Msimu uliopita, Azam iliiwakikisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kumaliza ligi kuu ikiwa mshindi wa pili, lakini ilitolewa raundi ya tatu. Iwapo Azam itaitoa Ferroviario,  itamenyana na mshindi kati ya St. Michel ya Shelisheli na ASSM Elgeco Plus ya Madagacar

Wakati huo huo, timu za KMKM na Chuoni za Zanzibar, zinaondoka nchini kwenda Ethiopia na Zimbabwe kwa ajili ya mechi zao za michuano ya klabu za Afrika.

KMKM imepangwa kumenyana na Dedebit ya Ethiopia mwishoni mwa wiki hii katika mechi ya michuano ya klabu bingwa itakayochezwa mjini Addis Ababa wakati Chuoni itamenyana na How Mine ya Zimbabwe katika mechi ya Kombe la Shirikisho, itakayochezwa mjini Harare.

KMKM ilitarajiwa kuondoka jana jioni kwenda Ethiopia kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia wakati Chuoni inatarajiwa kuondoka leo alfajiri kwenda Zimbabwe kwa ndege ya Shirika la Ndege la Zimbabwe.

Thursday, February 6, 2014

MARCELO ABAGULIWA





Shabiki mbaguzi ameonyesha ishara ya kibaguzi kwa beki wa Real Madrid, Marcelo.
 
Ishara hiyo ya kibaguzi amefanyiwa Marcelo raia wa Brazil wakati timu hiyo ilipokuwa inapambana na Atletico Madrid kwenye Kombe la Mfalme, jana.

Tayari Shirikisho la Soka la Hispania limeanza kulishughulikia suala hilo.

WAAMUZI WANAKOSEA KATIKA MECHI ZA TIMU KUBWA TU??



Baraka Mbolembole

WAAMUZI, hivi sasa wamekuwa kero kubwa kwa wapenzi wa soka nchini kutokana na kuboronga kwao katika michezo mbalimbali ya ligi kuu inayoendelea nchini. Abdallah Kambuzi, mwamuzi huyu alichezesha mchezo kati ya Yanga SC na Mbeya City, jumamosi iliyopita alionekana kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Si yeye tu kumeibuka malalamiko zaidi kutoka kwa timu nyingine kuhusu uchezeshaji mbaya wa waamuzi wengi nchi.

Nao ni binadamu, hivyo kufanya makosa ni jambo la kawaida. Kama mchezaji hufanya makosa na kuadhibiwa, hivyo mwamuzi nae anaweza kufanya makosa. Ila pamoja na adhabu mbalimbali ambazo wamekuwa wakipata bado hali si nzuri. Wamekuwa wakifanya makosa  kwenye mechi za Yanga, Simba na Azam FC, tena ni makosa ya makusudi kabisa. Mfano, ni kadi nyekundu ambayo alipewa kiungo wa City, Steven Mazanda wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Yanga, na matukio ambayo yalifanywa na Haruna Niyonzima, baada ya kiungo huyo wa Yanga kuwa na kadi ya njano, baadae alitakiwa kuondoshwa uwanjani kwa kadi ya pili ya njano ila haikuwa hivyo, mwamuzi akaamua kukataa bao lililokuwa halali la Hamis Kizza kama  njia ya kusahihisha makosa yake.

WANAPANGA MATOKEO?

Bado hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuhusu hilo, ila  timu nyingi zimekuwa zikiandaa 'fungu' la marefa ili wapate upendelo. Katika mchezo wa Ntibwa Sugar na Simba, kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime alionekana kuwa na jabza kuhusu uamuzi wa mwamuzi , Deonisia Kyura ambaye alimtoa nje kiungo na nahodha wa timu yake Shaaban Nditti. Awali Nditti alikuwa na kadi ya njano ila aliamua kumchapa kofi Amis Tambwe ambaye alimbana na miguu walipokuwa wameanguka wote chini.

Nditti, inadaiwa alitoa lugha chafu kwa mwamuzi huyo ndiyo maana akaadhibiwa, ila muda mwingi alionekana kushindwa kuendana na ukubwa wa mechi. Kwa nini alipangwa? Tafakari....
Bahati mbaya ni kuwa waamuzi hao wamekuwa wakilalamikiwa zaidi katika michezo dhidi ya timu kubwa tu, huku wanapokuwa wakichezesha michezo dhidi ya timu nyingine nje ya Yanga, Simba na Azam wamekuwa wakifanya vizuri. 
WANACHEZESHA KWA KUFUATA MAELEKEZO...
Ndiyo ukweli ulivyo, ila ni vigumu mtu wa Yanga, Simba au Azam kusema kuwa wanakuwa wakipata ' mbereko' kutoka kwa waamuzi. Tatizo hili linajulikana na wahusika ni viongozi wa klabu, waamuzi na wasimamizi wao. Klabu ndiyo zimekuwa zikihusika moja kwa moja kwa nia ya kupata matokeo ya ushindi tu. Mambo haya yanakera. Waamuzi nao ni binadamu hivyo ni rahisi kuingia katika ushawishi wa kuchukua pesa zinazowekwa mezani na viongozi wa klabu.
Mambo haya naamini yanafahimika kwa wahusika hivyo wanatakiwa kuchukua hatua ya haraka ya kuachana na mambo hayo ili kufanya timu zetu zishinde kwa uwezo wao, na mwisho tupate mabingwa sahihi. Siku zaidi ya 100 za rais wa TFF, Jamal Malinzi, soka la Tanzania bado lipo majaribuni. Waamuzi ni changamoto nyingine kubwa kwake. Awakataze kuchezesha kwa maagizo kutoka nje ya uwanja.

SIMBA WAENDA TANGA LEO

Timu ya soka ya Simba Sc, ipo njiani kuelekea mkoani Tanga tayari kabisa kuwavaa wanajeshi wa Jkt Mgambo.

Katika mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa mkwakwani, Kikosi hicho cha kocha Zdravko Lugarusic kitalazimika kucheza kufa au kupona ili kuweza kupata points tatu muhimu , baada ya Jana kuacha points mbili katika uwanja wa Jamhuri,.

Simba. Jana ililazimishwa sare na Mtibwa Sugar, baada ya kuwa nyuma kwa goli 1-0 kwa takriban dakika 40, baada ya Mussa Hassan Mgosi, kuitikisa Ngome ya ulinzi ya Simba Sc mnamo dakika ya 9 tu ya mchezo huu,.

Shukrani kwa mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye alifanya kazi ya ziada kipindi cha pili, kuisawazishia kikosi hicho cha Msimbazi.

Wednesday, February 5, 2014

SIMBA VS MTIBWA KATIKA PICHA


Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba Kilichoanza Dhidi ya Mtibwa leo
Nyuma Kuanzia Kushoto: Kocha Msaidizi Seleman Matola,Tambwe,Amri Kiemba,Joseph Owino,Jonas Mkude,Musoti.Mbele Kushoto:Singano,Awadhi,Haruna Chanongo,Ivo Mapunda,Rashid Baba Ubaya,Haruna Shamte.
 Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Nyuma kuanzia Kushoto:JumaLuizio,Shaban Nditi, Hassan Ramadhan,Ally Shomary  Salim Mbonde.Mbele Kuanzia Kushoto : Jamal Mnyate,Said Mkopi,Shaban Kisiga, Husein Sharif,Salvatory Mtebe,Mussa Mgosi.
Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
 Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.
 Kipa wa Mtibwa Hasani  Sharifu  
 Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo wakishangilia muda wote wa Mchezo

 Golikipa wa Timu ya Mtibwa Sugar Hussein Sharif Akiwa Ameokoa Moja ya Purukushani katika Lango Lake.Akishihudiwa na Beki wake Salim Mbonde Pamoja na Mshambuliaji wa Simba Khamisi Tambwe.
 Simba wakishangilia Goli lao lilofungwa na Khamis Tambwe Bao lililofungwa dakika 50 ya mchezo.

Mpira Umemalizika Mtibwa 1 -1 Simba. Goli la Mtibwa Sugar Lilifungwa dakika ya 18 ya Mchezo bao Lililofungwa na Mussa Mgosi .Hadi Mapumziko Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa Goli Hilo Moja.Kipindi cha Pili Mpira ulianza kwa kasi Simba walishambulia Lango la Mtibwa mara kwa mara Na kujipatia bao la Kusawazisha katika dakika ya 50 ya Mchezo.Katika Mchezo Mchezaji wa Mtibwa Shaban Nditi Alionyeshwa kadi Nyekundu Dakika ya 69 baada ya Kutoa maneno Machafu kwa Mwamuzi.Dakika ya 72 Said Ndemla anaingia Kuchukua nafasi ya  Haruna Shamte,Dakika ya 75, Juma Mpakala Aliingia Kuchukua nafasi ya  Jamal Mnyate. Dakika ya 87  wanafanya mabadiliko ya mwisho, aliingia Abdallah Salum Kuchukua nafasi  Mgosi..

FULL TIME , SIMBA 1-1 MTIBWA

MATCH LIVE CENTRE: MTIBWA SUGAR 1 - 1 SIMBA SC FULL TIME


Dakika ya 90, Mtibwa 1 -1 Simba. Kiujumla mechi haikuwa ya kuvutia sana kutokana na pitch mbovu ya uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro. Mtibwa wamepata kona dakika ya mwisho ila haikutoa matunda. Mechi imekwisha kwa sare ya bao 1-1

Dakika ya 87, Mtibwa 1-1 Simba. Mtibwa wanafanya mabadiliko ya mwisho, anaingia Abdallah Salum anatoka Mgosi

Dakika ya 84, Simba wanapata kona ila haina madhara

Dakika ya 78, Hassan Ramadhani anapewa kadi ya njano

Dakika ya 75, Juma Mpakala wa Mtibwa ameingia mahala kwa Jamal Mnyate

Dakika ya 72, Mtibwa 1-1 Simba- Said Ndemla anaingia mahala kwa Haruna Shamte

Dakika ya 69, naodha wa Mtibwa, Nditti anaoneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa uwanjani

Dakika ya 67, Mtibwa wanafanya mabadiliko ya kwanza, Vicent Barnabas anaingia Juma Luizio anatoka. Timu zinashambuliana ila Simba wanashambulia zaidi

Dakika ya 65, Mtibwa hawajafanya mabadiliko hadi wakati huu, Simbaw ameshafanya mabadiliko ya wachezaji wawili. Makipa wote wapo likizo

Dakika ya 60, Mtibwa 1-1 Simba. Mtibwa wanaonekana kupunguzwa kasi

Dakika ya 58, Simba wanaonekana kubadili stahili ya mchezo na kucheza mipira mirefu ili kuendana na hali ya uwanja

Dakika ya 55, Mtibwa 1-1. Mpira umeanza kuwa na kasi

Dakika ya 52, Uhuru Suleiman anaingia kuchukua nafasi ya Chanongo kwa upande wa Simba

Dakika ya 50 , GOOOO, Tabwe , Mtibwa 1-1 Simba

Dakika ya 48, Mtibwa 1- 0 Simba

Dakika ya 46, Tambwe anapoteza nafasi. Simba tayari wamefika mara mbili katika lango la Mtibwa

Dakika 45 za kipindi cha pili zinaanza. Mtibwa ndiyo wanaanza mpira

Goli la Mtibwa Sugar limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mussa Hasan Mgosi.

Dakika 45 , mpira ni mapumziko . Katika kipindi hiki Mtibwa wamecheza kwa kufuata maelekezo, huku Simba wakionekana kupoteza mawasiliano wao wenyewe, japo uwanja unaonekana kuwasumbua kwa kuwa mpira hautulii.

Dakika 44, Nditti anapata kadi ya njano

Dakika 43 mpira umesimama, Mkopi amepata maumivu tena

Dakika ya 40, Mtibwa 1-0 Simba

Dakika ya 39 Mtibwa wanapata faulo ila wanapoteza

Dakika ya 36, Awadh Juma anatoka anaingia Ally Badru upande wa Simba

Dakika ya 34, Simba wanapata kona Mkude anapiga fyongo

Dakika ya 28, Mtibwa bado wanawabana sana Simba, hawawapi nafasi ya kucheza

Dakika ya 28, Mtibwa bado wanawabana sana Simba, hawawapi nafasi ya kucheza

Dakika ya 26, Mtibwa 1-0 Simba. Uwanja wa Jamhuri sehemu ya kuchezea si nzuri.

Dakika ya 22, Shaaban Nditti na Kisiga wameonekana kumiliki eneo la kiungo.

Dakika ya 20, Mtibwa  1-0 Simba

Dakika 17, Amri Kiemba anaunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Issa Rashid ila unatoka nje

Dakika ya 15, Simba wamepata kona moja, ila haikuzaa matunda. Mtibwa wanacheza soka la nguvu kuliko Simba. Wachezaji, Jamal Simba, Shaaban Kisiga, Mgosi, na Luizio wanawasumbua sana walinzi wa Simba

Dakika ya kumi mpira bado unachezwa bila mipango. Tayari Simbawamecheza faulo tatu. Mtibwa wanapata bao la kuongoza lililofungwa na Mussa Hassan Mgosi. Ni makosa ya kipa Ivo Mapunda

Dakika ya sita, kipa Husein Shariff anadaka mpira wa kwanza uliopigwa na Amis Tambwe
Dakika ya pili, Mtibwa wanapata faulo, Said Mkopi anapiga ila wanapoteza

Dakika ya kwanza mpira umeanza hapa uwanja wa Jamhuri, Simba ndiyo wameanza mpira . Juma Luizio anafanya shambulizi la kwanza

Tuesday, February 4, 2014

MALINZI ATEMBELEA RUANGWA



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametembelea Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka huu), pia alikuwa mgeni rasmi mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull City na Mbagala City, na kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na uamuzi kwa Wilaya ya Ruangwa.

RAMBIRAMBI MSIBA WA OMARI CHANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Vijana, Moro United na Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi (Februari 1 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Changa wakati wake uwanjani akichezea timu mbalimbali, alitoa mchango mkubwa ambao tutaukumbuka daima.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Changa, klabu ya Moro United na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. 

Katika maziko, TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kidao Wilfred, na imetoa rambirambi ya sh. 200,000.

MASHABIKI MBARONI KWA TIKETI FEKI



Mshabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.

Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchini.

Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa. Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.

TFF YASITISHA MATUMIZI YA TIKETI ZA ELECTRONICS




Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina kabla ya kuendelea tena.

Uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana (Februari 3 mwaka huu) katika ofisi za Shirikisho.

Tathmini hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni hadhari iliyotolewa na vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.

Tayari zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi ya kununua na kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia uwanjani na washabiki wengi kununua tiketi dakika za mwisho hivyo kuchangia misongamano.

PAWASSA, RWEYEMAMU WATEULIWA KUSAKA VIPAJI




 


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).


Makocha hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo zaidi.

Walioteuliwa ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri (Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani (Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).

Elly Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar), John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es Salaam).

Kenny Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera (Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).

Peter Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Sebastian Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan (Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es Salaam).