Timu ya taifa ya visiwa vya Zanzibar maarufu kwa Zanzibar Heroes, kesho wanatarajiwa kutupa karata ya pili dhidi ya Ethiopia katika muendelezo wa Michuano ya Cecafa Challenge Cup.
Timu hiyo inayoundwa na Baadhi ya Chipukizi kutoka Simba Sc, inakutana na mtihani mgumu dhidi ya wawakilishi hao bora wa michuano ya kutafuta timu zitakazofuzu Kombe la Dunia nchini Brazil.
Katika mechi iliyopita, Zanzibar Heroes iliwalaza timu ya Sudan Kusini kwa jumla ya goli 2-1.
No comments:
Post a Comment