ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, September 26, 2013

Kamwaga;Okwi ni mali ya Etoile, tunachohitaji kwa sasa ni fedha zetu

Msemaji wa wekundu wa msimbazi Ezekiel Kamwaga, amesema kuwa Emanuel Okwi
ni mali ya Etoile na wao kama wao kama Simba wanachohitaji ni fedha zao.
Kamwaga katika taarifa yake aliyotoa kwa vyombo vya habari,amesema kuwa Simba haina haki ya kufanya mawasiliano wala kuzungumza na Okwi bila ridhaa ya Etoile de Sahel. Hii imekuja siku chache baada ya mshambuliaji huyo raia wa Uganda kuonekana mitaa ya jiji la Dar es salaam pia kwenye mchezo wa mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City, Okwi ni mali ya Etoile na sisi kama Simba tunachosubiri ni fedha toka kwao ambazo walituahidi watazilipa ifikapo mwishoni wa mwezi huu wa tisa, iliongeza taarifa hiyo.

Emanuel Okwi ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda ambaye alifanya makubwa akiwa na Simba kiasi cha mashabiki kumkumbuka sana na kuomba arudishwe Simba baada ya kuonekana hayuko sawa na uongozi wake w klabu ye Etoile

No comments:

Post a Comment