ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, September 26, 2013

Simba B waendelea na mazoezi leo

Kikosi kipya kabisa cha Simba B chini ya kocha wake Selemani Matola na meneja Patrick Rweyemamu,leo kimeendelea kujifua katika viwanja vya mwenge.
Timu hii inayosukwa upya baada ya wenzao kupandishwa kwenda A,kinajiandaa na mechi ya kirafiki itakayopigwa siku ya jumapili kabla ya kuwapisha kaka zao kucheza na JKT Ruvu, mechi hiyo itapigwa muda wa saa 8.00 mchana katika siku hiyo

Simba B, imejiwekea historia ya peke yake ikiwa ya kwanza na ya mwisho mpaka sasa kuchukua ubingwa wa Banc ABC super 8 iliyofanyika msimu uliyopita, ubora wa timu hii ulithibitishwa pale
ilipowafunga vigogo wa soka la Tanzania kama Azam FC na wenzao Mtibwa ya Morogoro

No comments:

Post a Comment