ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, August 15, 2014

AYOUB MZEE KUTOKA SIMBA SC MPAKA KUIBEBA DUNIA,SALAAM KWA UONGOZI





FAIR PLAY, FAIR PLAY, FAIR PLAY haya mabango hutawala viwanjani popote panapohusika FIFA, hili neno hata sisi huliimba kila kukicha, "michezo furaha, michezo udugu, michezo amani".
Hebu angalia kwa makini hiyo picha hapo chini, hii picha niliikuta kwenye group yetu ya Kandanda kuna mdau Lawrence Joseph Mwonyonyi aliiweka huku akiambatanisha na swali je, mnawafahamu hawa waliopo kwenye picha? Wakati majibu yakitolewa nilipatwa na mshtuko mkubwa, niliingiwa na fadhaa mwili ulikufa ganzi, machozi yalinilenga, AYOUB MZEE??? Awali nilipinga nikisema hawezi kuwa Mzee ghafla hivi, ndipo nilipopata habari kuwa huyu bwana sasa hivi ni mwendawazimu, ghafla nikakimbuka kikosi hiki cha Nyota Nyekundu ama Red Stars (kumbuka hii ndio timu pekee iliyokuwa ikit
ambulika kwa majina yote mawili achili mbali yale majina yenu fake, "Msimbazi" na "Jangwani. 1) Morris Nyuchi, 2) John Bosco 3) Rafael Mapunda 4) Mohamed Nyauba 5) Pazi Ally 6) Faustin Kibingwa 7) Roster Ndunguru 8) Hamisi Dilunga 9) Steven Chibichi 10) Ayuob Mzee n.k.
Ayoub Mzee alikuwa ni mchezaji mahiri wa Nyota Nyekundu baadaye akahamia Simba SC mwanzoni mwa miaka ya 90, katika moja ya michezo yake akiwa pale Simba SC aliwahi kupatwa na mkasa wa kupigwa kichwa cha nyuma (medulla oblongata) na mchezaji wa Coastal Union (sasa ni marehemu), hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili akiwa hajitambui hakika baada ya hapo sidhani kama alirejea tena kwenye soka la ushindani na sikupata kusikia tena habari zake hadi hii juzi kwenye hii mitandao ya kijamii, inasemekena ugonjwa huu wa wendawazimu ulichangiwa pia na kichwa kile.
Mimi ni muumin wa Fair Play siwapendi wachezaji wote wasiotii kanuni za mchezo, ambao wako tayari kuharibu kabisa Carrier ya wenzao katika soka, mchezo usio salama viwanjani si tu unaigharimu timu yako bali pia unaweza kuharibu kabisa maisha ya mchezaji mwenzio, unaweza kumpa kilema cha maisha!!, Marehemu baba yangu alipata kunisimulia wakati ule wa Gossage Cup (Taifa Cup) kuna mchezaji wa timu ya mkoa wa Iringa alichezewa rafu mbaya sana pale Karume Stadium, alivunjika miguu yote miwili hali iliyompelekea kuwa kilema aliporejea kwao Iringa alijiua unaweza kusema eti ndio utamaduni wao la hasha nadhani yeye aliangalia maisha yake akaona kuwa yameshaharibika kabisa, mtu uliyekuwa ukitembea mwenyewe leo unahitaji msaada wa mtu mwingine??
Vijana mnaocheza soka hivi sasa najua mko wengi humu, viongozi wa vilabu najua mko wengi humu hata vingozi wa TFF najua mko humu ni wakati sasa wa kueleweshana zaidi ni kwa nini FIFA wanahimiza FAIR PLAY si wimbo tu kama tunavyoimba zile nyimbo za Taifa.
( Huyo mwingine pichani kushoto ni Lusajo Mwamakula aliyepata kuwa Nahodha wa Nazareth ya Iringa) 
Picha kwa hisani ya Lawrence J. Mwonyonyi.
Wakatabahu, Ijumaa Karim

No comments:

Post a Comment