ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, October 30, 2013

Simba kujiuliza kwa Kagera leo

Baada ya kuandamwa kwa sare na hatimaye kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Azam katika muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara, timu ya Simba Sc Leo kwa Mara nyingine itashuka katika uwanja mkuu wa taifa kuumana na timu isiyotabirika ya Kagera Sugar.

Simba ambayo ina Lundo la wachezaji waliopelekwa timu B, huku ikionesha udhaifu katika safu ya Ulinzi, inalazimika kupigana kwa hali na Mali Leo, ili iweze kupata points 3 ambazo zitaifanya angalau ifufue matumaini ya kuwemo kwenye timu zenye nafasi ya kutwaa taji Hilo mwaka huu.

Wakati Huohuo , mshambulizi Amissi Tambwe anatarajia kuwaongoza wenzake katika mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment