ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 12, 2013

SIMBA YAIFUMUA PRISONS

Bao pekee la kiungo wa kimataifa wa Tanzania Jonas Mkude kutoka nje kabisa ya kumi na nane, leo limetosha kuizamisha timu ya wajelajela wa Prisons ya Mbeya katika uwanja mkuu wa Taifa.

Simba ambayo leo ilihitaji ushindi ili kuzidi kujiimarisha kileleni, ilibidi isubiri mpaka dakika ya 63 pale kiungo wake huyo alipoachia shuti kali kabisa lililomshinda kipa wa Prisons.

Katika mchezo wa leo, Simba ilibidi iwapumzishe wachezaji wake nyota ambao watawasubiri watani wao wa jadi Yanga hapo siku ya Jumapili,.

No comments:

Post a Comment