ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, October 11, 2013

SIMBA KUJIULIZA KWA PRISON LEO TAIFA

Baada ya wiki ngumu iliyochagizwa na kutoa sare dhodi ya Ruvu Shooting siku ya jumamosi iliyopita, timu ya Simba leo itawavaa maafande wa Prison ya Mbeya katika mechi itakayopigwa katika uwanja wa taifa.
Mechi hiyo inayosubiriwa  kwa hamu na mashabiki wa Simba, inatarajiwa kuwa yenye msisimko wa aina yake kutokana na ushindi wa mechi ya mwisho waliocheza Prison, huku Simba ikitumia mchezo huo kama kujiandaa na mechi dhidi ya mtani wake Yanga SC.

Simba iliwarudisha wachezaji wake mahiri kwenda kucheza timu B, kwa kile kilichoitwa utovu wa nidhamu na kutojituma kwa wachezaji hao, wachezaji waliopelekwa timu B ambao hawatakuwepo katika mechi ya leo ni Henry Joseph, Rashid Ismail, Ramadhan Chombo.

Kocha Abdallah Kibaden amesema kuwa  mechi hiyo itakuwa ngumu ingawa atajitahidi kuibuka na ushindi leo ili timu yake iweze kuzidi kukalia kiti cha uongozi.

No comments:

Post a Comment