ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 31, 2013

Simba Yamalizwa Taifa leo

Timu ya Simba Sc, Leo imelazimishwa sare na timu ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa taifa!

Timu hiyo ya jijini Dar Es Salaam,ilikuwa mbele kwa goli 1-0 la dakika ya 45, lililofungwa na mrundi Amissi Tambwe baada ya kupokea pasi ya Bentram Mombeki na kumpiga chenga Beki Salum Kanoni.

Kwa ujumla timu zote zilishambuliana kwa Zamu ingawa Kagera Sugar walionekana bora zaidi ya watoto hao wa Msimbazi.

Wakati Huohuo ,uwanja wa taifa Leo ukigeuka.kuwa uwanja wa vita baina ya polisi na mashabiki wa Simba Sc, hii ilitokea baada ya muamizi Mohamed Theofile toka Morogoro kuwapa Kagera penati ya utata ambayo Mshambuliaji Daud Jumannealifanyiwa madhambi nje ya eneo la penati, lakini la ajabu muamuzi huyo aliamua lipigwe pigo la penati ambalo lilikwamishwa kiufundi na Beki Salum Kanoni!


No comments:

Post a Comment