ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 31, 2013

Simba hii ya Kibaden ni ya ajabu!

Jana siku ya alhamisi, uwanja wa taifa uligeuka eneo la vita baina ya polisi na mashabiki wa Simba baada ya mchezaji wa zamani wa timu hiyo Salum Kanon kuingiza kimiani penati iliyotolewa dakika ya 92 na muamuzi Mohamed Theofil toka Morogoro.

Vurugu za mashabiki hao ziliambatana na ung'olewaji wa baadhi ya viti katika uwanja huo mkuu wa taifa,hakika ilisikitisha sana.

Simba SCinayofundishwa na kocha mzalendo Abdallah King Kibaden haikustahili kuwa nafasi ya nne kama ilivyo sasa kama na kama tu haki katika soka ingefuatwa, nasema hivyo kutokana takriban mechi zote alizocheza katika nusu ya kwanza ya msimu nimeziona kasoro ile ya Ashanti ambayo bado haijachezwa.

Timu hii yenye makao yake mtaa wa msimbazi,inaonekana haina jipya katika maeneo yote ya uwanjani pale inapocheza, ukiachilia mbali kuwa na wachezaji wenye vipaji, timu kiujumla haina jipya huku ikiwa na defence dhaifu, viungo wasiofanya kazi kwa ufasaha, na washambuliaji wanaotegemea juhudi zao binafsi kuweza kupata magoli.

Ikumbukwe timu hii kabla ya ligi kuanza, plan ya Simba ilikuwa ni kupandisha kizazi chote cha kina Ndemla kwenda kufanya kazi timu A, kweli ilifanikiwa kimaandishi,nasema Simba ilifanikiwa kimaandishi kwa kuwa waliokuwepo kambini kwa kizazi hiki sio wote, wengine wapo tu mtaani, yuko wapi Marcel Kaheza? Yuko wapi Rashid Mkoko? nk

Takribani wachezaji wasiozidi nane ndio wapo kambini na wenzao, wakati wengine wanapotezwa kimakusudi. Nani asiyeijua kasi ya Ramadhani Kiparamoto ila ukiulizia unaambiwa nidhamu yao ni ndogo.

Nidhamu ipi wanayoitaka makocha wetu wakati timu inafanya vibaya? Huwezi kuuulaumu uongozi wakati timu inafanya vibaya huku ukisimamisha baadhi ya wachezaji na kuwa na chaguo dogo tu pale timu inapozidiwa, sitaki kuamini kama Kibaden anafundishia Simba kwa historia inayombeba,pia sitaki kuamini kama kocha wetu ameshindwa kazi.

Uongozi ulionesha udhaifu wa hali ya juu, pale ulipoamua kuachana na Juma Kaseja huku ukimsajili kwa mkataba wa ajabu Andrew Ntalla ambaye hana msaada zaidi ya kukaa jukwaani kama mimi pale uwanjani, dhambi ya kubaguana katika timu, dhambi ya kila mwenye mawazo ya faida kuambiwa anaihujumu timu, dhambi ya wadau kuogopa kusema ukweli na kukubali kuburuzwa wakati timu haichezi vizuri matokeo yake ndio haya.


Ikumbukwe kuwa,hakuna miujiza kwenye soka ni mipango thabiti na watu thabiti,kuisimamia Simba Sc ikacheza kwa burudani, ushindi utakuwa rahisi sana kuliko vile watu wanavyofikiria.

Ila tuliamua kuchukua njia hii,wacha tujifunze kwanza inawezekana tukaja kupata akili na uelewa juu ya maamuzi yetu yasiyo na busara kwa timu yetu.

No comments:

Post a Comment