ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, August 11, 2014

SPS KUZINDUA LOGO YAKE KATIKA TAFRIJA YA UZINDUZI WA TAWI LAKE

Simba Platinum Supporters (SPS), imepanga kuzindua logo yake rasmi ikiendana na tafrija ya kuzindua tawi lao.
Akiongea na muandishi wa habari hii, Mwenyekiti wa Simba Platinum Supporters amesema kuwa wadau wa Simba SC wameoneshwa logo mbili ingawa kwenye kampuni ya usajili wa logo zimepelekwa tatu" Ndio tumeonesha logo mbili tu, ingawa kule tumepeleka logo tatu ili watupitishie moja ambayo itakuwa ya msingi kwetu sisi" aliongeza.

Alipoulizwa kwanini wadau wa SimbaSC waoneshwe logo mbili badala ya zote Mrs Amina Poyo ambaye ndiye mwenyekiti alijibu kuwa" tumeamua hivi kwa kuwa tunataka logo moja lazima ipite, tungezionesha zote yawezekana kungekuwa na mgongano wa logo za aina moja"


Katika kurasa na mitandao ya SPS kwa jana usiku," kulichafuka " logo mbili za maana ambazo supporters hao wa Simba SC wanataka kuzifanyia kazi.

No comments:

Post a Comment