ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, March 23, 2014

SIMBA YAJITOA RASMI KATIKA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Kikosi cha Simba SC, leo kimejitoa rasmi katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kupokea kichapo cha goli 1-0, kutoka kwa Coastal Union ya Tanga.

Ikicheza soka dhoofu, Simba Sc ilionekana kubanwa katika kila idara hali iliyosababisha timu hiyo kupoteana kwa muda wote.

Wakati huo huo kiungo wa Simba Sc Ramadhan Singano Messi amejikuta anashindwa kuzuia hasira zake baada ya kuupiga teke mlango mmoja wa uwanja wa taifa hali iliyopelekea kuvunjika kwa mlango huo.

No comments:

Post a Comment