ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, January 28, 2015

DRFA YAOMBA WAPENZI KUJITOKEZA KWA WINGI KUZISHANGILIA TIMU ZA DAR ES SALAAM


FRIENDS RANGERS KUTOKA DAR ES SALAAM INAYOSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA NA INA MATUMAINI YA KUINGIA LIGI KUU BARA.
Uongozi wa Chama  cha Soka Dar es Salaam (DRFA), umewaomba, mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki Ligi Kuu Daraja la Kwanza na michuano ya Taifa Cup ya wanawake.

 Msemaji wa DRFA, Omar Katanga amesema pamoja na timu za Ligi Daraja la Kwanza, lakini DRFA wamesisitiza kuwa hata zile za Ligi Kuu Bara kutoka Darm zinapaswa kuungwa mkono.

Leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuna mechi ya Uwanja wa Taifa na Simba pia ni timu chini ya DRFA ambayo imesisitiza nayo ishangiliwe.

Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita, Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake, mechi zote zilikuwa sare. 

Katika michuano ya taifa Cup, Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali zilizopigwa jana.

Temeke imeiangamiza bila huruma Mbeya mabao 3-0 na Ilala ikiizodoa kiana Iringa kwa mabao 2-1.

Aidha, DRFA imeipongeza timu ya Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya makundi.


No comments:

Post a Comment