ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, January 28, 2015

HISIA ZA AGNATUS OBEL NDANI YA SIMBA SC


Agnatius Obel 


Huko Ujerumani kuna timu inafanya
vibaya kuliko Simba, ni Borrusia
Dortmund, ni wa pili kutoka
mwisho....lakini bado wana Kocha yule
yule waliyeanza nae msimu!
Hapa kwetu Simba imeshafukuza Kocha
mmoja, na bado matokeo ni mabaya na
kuna uwezekano yakaendelea kuwa
mabaya!
Tofauti iliyopo kati ya Simba na Borrusia
ni, nani anaamini nini??
Kwa Borrusia washabiki na hata wadau
wanaamini ni kipindi cha mpito japo pia
wanaweza kufukuza Kocha na wao,
lakini hapa kwetu ni mwiko kuwa na
kipindi cha mpito au kusema mambo ya
mpira, ni lazima Simba ishinde na kukaa
juu!!
Ofcoz kokote pale, kama timu haifanyi
vizuri lazima Kocha atawajibika, na
kuangalia mambo mengine, lakini pia si
kila wakati timu inapofanya vibaya basi
ni tatizo la Kocha!
Hakuna tasnia ninayoichukia kama ya
habari hasa za michezo hapa Tanzania,
hakuna weledi, wanahongwa, hawafanyi
utafiti kwa kina, ni watu wa kupelekwa
pelekwa tu!
Hakika wanaiharibu jamii sio siri,
inakubidi uwe smart sana ili usiingie
kwenye mkumbo wa kuhadaika!!
Nina maana kusema hivi, ni kweli Simba
ina matatizo, ukiwa unaujua mpira
ukiiangalia tu Simba unajua ina
mapungufu, lakini pia hata mpira wa
hapa una mapungufu tena mengi tu, kwa
hiyo pamoja na mapungufu ya Simba
bado inaweza kufanya vizuri!!
Waandishi wa habari, kama kuna mtu
walikuwa wanamsakama kila kukicha
basi alikuwa Rage, japo cha kushangaza
hakuwahi kuwa kwenye mwenendo
mbaya kama huu!!
Waandishi wa habari, wanaiaminisha
jamii kwamba Friends of Simba ndio kila
kitu Simba.........je wameshafanya
uchunguzi wa kutosha kwenye hili??
Basi hata washabiki wa Simba nao
wanaamini hivyo, na kibaya zaidi
wamefungwa likishindikana kwa Friends
of Simba ndio basi tena!!
Kwa mtu yoyote anayeangalia mpira kwa
umakini na kuufahamu pia, Simba wana
matatizo ya, Golikipa mahiri, beki wa
kati, kiungo mshambuliaji na
mshambuliaji!!
Mpira kila mtu ana jinsi anavyoutazama,
siwezi kuelezea kwa mapana sana kwa
nn nazungumzia hizo nafasi, lakini
wanasema mpira ni mchezo wa wazi
hakuna cha kujificha!
Kwenye timu lazima uwe na wachezaji
wasiopungua watano ambao ni
'outstanding perfomer' hata kama siku
wanakuwa wako vibaya basi wenzao
wanawabeba!!
Niseme tu, ni Mkude pekee ndiye
mchezaji mahiri na anaweza kucheza na
watu wa aina yoyote kwa sasa,
wachezaji wengine wanapanda na
kushuka, kitu ambacho kwenye timu
iliyopo kwenye ligi ni majanga!!
Tatizo la Tanzania ni kutofautisha ni
aina gani ya wachezaji wanaofaa
kushindana na kuleta mafanikio na
wachezaji wenye uwezo kupiga chenga
na visigino, Simba kuna wachezaji wengi
sana katika suala la kuchezea mpira ni
mahodari lakini je wanaisaidia timu
ipasavyo kwenye ligi??
Simba ya Aveva imemruhusu Tambwe
aondoke kwa sababu wanazojua wao
lakini si za kisoka naamini, bado
walimwacha comanding center back
Musoti kwa ajili ya Okwi, sio mbaya
Okwi ni mzuri halina ubishi lakini ndio
tumkate Musoti bila kuwa na mbadala
wake?? Ikumbukwe Kaze Gilbert
alishindwa kucheza na Owino kwa
sababu ya type zao kulingana, ni kama
Hassan Isihaka na Juuko na Owino pia
ambaye ni kama ameonyeshwa mlango
wa kutokea, lazima apatikane mtu
mgumu mmoja!!
Lakini waandishi wa habari
hawaichambui Simba kama
walivyokuwa wakifanya wakati wa Rage,
ni kwa kuwa wanaamini Friends of
Simba ni kila kitu, lakini kama pia
walikuwa wakihongwa ili wamchafue
Rage ili aonekane hafai na leo
wanaomhonga wako madarakani,
unafikiri watafanyaje??
Sipati picha kama Rage angekuwa
madarakani, ni mara ngapi ungewasikia
wale wale, tuachie timu yetu, lakini leo
sio kwamba hawapo wapo ila kwa kuwa
Friends ndio kila kitu basi hewala!!
Uongozi ni busara pia, sitaki kuamini
sana mambo ya Ukawa, lakini kwa
utamaduni wa mpira wetu mambo ya nje
nayo si ya kudharau, lakini tumefikaje
hapa??
Kwani mbona watu wa Friends
wameshawahi kuongoza na bado Simba
ikawa moja, kwa nn sasa iko tofauti??
Friends wana uzuri na athari zake,
Aveva kama mtawala mzuri, kuna
mambo nina hakika hata yeye
hakupenda yatokee lakini kwa nguvu
aliyowapa Friends mambo yamemzidi,
hakuja asiyejua kama Phiri ilikuwa kama
kafara tu, na hata Aveva mwenyewe
imenukuliwa hakujua kama Phiri alifutwa
kazi wakati muafaka zaidi ya kupewa
taarifa tu!!
Nadhani Aveva hana cha kusema,na
wala asisuthubutu aonane na Ukawa na
kufanya Simba iwe moja!!
Sifurahii Ukawa hata kidogo, lakini
narudia tena nawachukia waandishi wa
habari, Simba imekuwa ikiumizwa sana
na Friends of Simba na kuhujumiwa pia
pindi Uongozi unaokuwa madarakani
hawaelewani, sasa imegeuka na wao
wanaionja joto ya jiwe, nadhani ndio
maana walijiamini kwamba wao wako
madarakani basi kila kitu sawa, lakini
wamesahau hizi timu zina wenyewe!
Tutasikia mengi sana☝☝

No comments:

Post a Comment