ASASH GENERAL TRADERS

Monday, August 8, 2016
MAVUGO AWAITA WANASIMBA TAIFA LEO
SIMBA SC KIBOKO YAO
![]() |
KIKOSI CHA VIONGOZI WA SIMBA SIKU YA SIMBA DAY 2015 |
Ndugu wanasimba, hilo linadhihirishwa na sapoti ya hali ya juu ambayo tumekua tukiitoa kwa timu yetu kwenye kila aina ya nyakati. Tumekua wamoja pamoja na changamoto za hapa na pale, tukipasua milima na mabonde na hatimaye nuru imeanza kuonekana.
Tupo katika hatua nzuri ya maendeleo ya kweli. Hatua ya mabadiliko ya mfumo wa klabu yetu ambao nia na madhumuni ni kuifanya iweze kujitegemea kiuchumi. Tena uchumi ulio thabiti na imara katika dunia ya sasa.
Pamoja na ukweli kwamba kwa miaka ya hivi karibuni tumeikosa ile Simba tunayoijua, lakini walau uwanja wetu wenyewe upo katika hatua nzuri tu na ninaweza kukuhakikishia kwamba utakamilika muda si mrefu. Tuwe na uwanja wa mazoezi wa kwetu wenyewe, ni kitu ambacho kilishindikana kwa kipindi kirefu na ni kitu ambacho hata wenzetu wengi wameshindwa kufanya.
Si nia yangu kueleza hayo leo, nia yangu ni kuwakumbusha jambo hili ambalo pia limekua likidhihirisha kwamba Simba ni klabu ya watu makini. SIMBA DAY ni sikukuu yetu Wanasimba ambayo naweza kusema ni tamasha kubwa la klabu katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki.
Hakuna timu yoyote ambayo imeweza kuwa na utaratibu kama huu, na hiki ni kitu ambacho wanasimba tunapaswa kujivunia. Ni kitu kinachotuunganisha sisi, viongozi wetu na wachezaji wetu.
Hii ni Simba Week, ambapo shughuli nyingi za kuelekea kwenye kilele cha siku yetu zinafanyika. Tunafanya usafi, tunatembelea wagonjwa, tunatoa misaada na mambo mengine mengi kwa jamii yetu. Lakini kilele cha yote haya ni Agosti 8 pale uwanja wa taifa
Kilele cha siku hii ni mechi kati ya Simba na FC Leopards kutoka Kenya lakini itatanguliwa na mambo mengi kama utambulisho wa jezi zetu mpya ambazo pia zitakua zikiuzwa pale uwanjani.
Tutazitambua namba za wachezaji wetu watazozitumia kwenye msimu mpya,
Lakini pia tutakiona kikosi chetu chote siku hiyo. Wachezaji wapya wakiwemo wale wa kimataifa pamoja na wazamani ambao kwa pamoja wataunda kikosi kipya cha Simba chenye kila aina ya matumaini, watatambulishwa mbele ya Wanasimba.
Hii ni fursa ya pekee ambayo inapatikana mara moja tu kwa mwaka. Fursa ya kuwaona wachezaji wote wakitambulishwa na kisha kuwaona uwanjani wakimenyana na AFC Leopards.
Kama wewe ni mwanasimba, njoo uwanja wa taifa Agosti 8 ili uwe sehemu ya Simba itakayoandika historia mpya.
Njoo uwe sehemu ya vuguvugu la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vilabu, mfumo ambao ni sisi tunaokwenda kuuanzisha hapa nchini. Tayari wapinzani wanaweweseka na wanatamani kuiga kwa sababu wanajua Simba akiwa imara anatisha kiasi gani.
Njoo tuongee ya kwetu, tuburudike kwa pamoja kama familia kwa sababu kutakua na burudani nyingi na show zilizoandaliwa na uongozi kwa ajili yetu.
Njoo tujivunie kua Simba,
Simba Nguvu Moja
Imeandikwa na Ally shatry (Bab chicharito)
Saturday, July 30, 2016
MO AIBUKIA MAZOEZINI SIMBA SC
Baada ya mchezo huo Kocha Joseph Omog wa Simba alisema, amefurahishwa na uwezo ulioonyesha na wachezaji wake huku akidai wapinzania wao walikuwa katika kiwango bora
Friday, July 29, 2016
MO KUWEKEZA BILIONI 20 SIMBA SC,,WANACHAMA WACHEKELEA
Monday, February 22, 2016
BANDA; ILIKUWA NGUMU ZAIDI KUPAMBANA TUKIWA PUNGUFU
Abdi Banda juzi alitolewa mapema katika mchezo ambao ulikuja kuwa wa hovyo baada ya kumgusa kwenye bega mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma,.
Katika hatua nyingine,ungozi wa Simba SC umewapa mapumziko ya muda mfupi wachezaji wake kabla ya kuivaa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa Machi 6.
Friday, March 6, 2015
7000 KUONA SIMBA DHIDI YA YANGA
Monday, March 2, 2015
KILOMONI ; MCHEZAJI PEKEE KUWAUA YANGA 4 KWA MIGUU YAKE
Mzee Hamisi Ally Kilomoni, mchezaji wa zamani wa Sunderland anayekumbukwa na Yanga kwa jinsi alivyokuwa anapachika mabao dhidi yao. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
SUNDERLAND, ambayo wakati huo ilikuwa ikishikilia ubingwa wa kandanda wa Afrika Mashariki ‘Allsopps Cup’ pamoja na ubingwa wa Taifa, Jumapili ya Mei Mosi, 1966 iliinyoa Yanga bila maji kwa kuifunga magoli 4-0 katika Uwanja wa Ilala, mbele ya waheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Mfaume Kawawa, Mawaziri, Mabalozi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Selemani Kitundu na maelfu ya watazamaji waliojazana hapo. Mara baada ya mchezo mashabiki wa Sunderland walilipuka kwa mayowe ya furaha huku wakiitania Yanga kuwa ni ‘Four-Four’ kwa kufungwa magoli manne bila majibu. Wakati huo gari za Peugeot 404 kutoka Ufaransa ndiyo kwanza zilikuwa zinaingia nchini.
Hii ilikuwa ni fainali ya kugombea Kombe la NUTA lililotolewa kushindaniwa maalum kwa sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, yaani May Day.
Mpira ulianza huku mvua ikinyesha na upepo mwingi ukivuma. Yanga ndio walioanza kuingia uwanjani wakipitia mlango usiostahili kupitiwa, lakini yote hiyo haikufaa kitu, kwani goli nne kwa yai ziliamua nani bingwa wa soka. Kipigo hicho kilikuwa kama cha kulipa kisasi baada ya Sunderland kufungwa 5-4 na Yanga hapo Machi Mosi katika fainali ya Kombe la Nyota.
Timu zote zilitambulishwa kwa mgeni wa heshima, Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Kawawa. Baada ya hapo mpira ukaanza huku Sunderland, Sanda au Abidjan, kama walivyokuwa wakiitwa, wakicheza mchezo wa haraka haraka (quick game) ili kuwachosha mabeki wa Yanga.
Zilipotimu dakika tatu tu mpira ukawa miguuni mwa Asmat, winga wa kushoto wa Sunderland, na hapo ikatumika ‘one touch’, akamlamba chenga Abuu Mapyopyo wa Yanga na kumpasia Hamisi Kilomoni, ambaye alimzungusha Athumani Kilambo wa Yanga na kisha akampasia Mustafa Choteka, naye bila kuchelewa akammegea Haji Lesso, ambaye alifumua shuti kali la ‘mwana-ukome’ huku akiwa kafumba macho. Alipofumbua akapashwa habari kwamba mpira umetikisa nyavu za Yanga.
Haukupita muda mrefu Mustafa aliutupa mpira hadi kwa Haji, ambaye kwa mara nyingine tena bila kufanya makosa akafunga goli la pili kwa Sunderland. Mpira uliendelea huwa wa vuta-nikuvute hadi kilipomalizika kipindi cha kwanza.
Wakati wote huu Sunderland walikuwa wakitumia staili zao mpya za ‘Abidjan’. Watu wengi walikuwa hawajui jinsi staili za Abidjan zinavyochezwa, lakini siku hiyo walijionea wenyewe, yaani mfungaji magoli huwa mmoja tu naye ni ‘Insaidi’ au ‘sentafowadi’. Ndivyo ilivyokuwa siku hiyo, kwani Haji ndiye aliyefunga magoli mengine mawili katika kipindi cha pili na kuipatia timu yake ushindi mnono dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Yanga.
Siku hiyo timu zilipangwa hivi:
YANGA: Saad Mohammed Songambele, Abuu Mapyopyo, Omari Kapera, Athumani Kilambo, Juma Washokera, Awadh Gessani, Kassim Lengwe, Mfamau, Peter Mandawa, Mtumwa Mgeni, Mwinyiamiri Mwinyimadi.
SUNDERLAND: Mbaraka Salum Magembe, Tayari Mussa, Mussa Libabu, Yussuf Omari Kimimbi, Gilbert Mahinya, Adam Athmani, Abdu Rashid Kibunzi, Hamisi Kilomoni, Haji Lesso, Astmati, Mustafa Choteka, Arthur Mambetta.
Mwamuzi alikuwa Marijani Shabani Marijani aliyesaidiwa na Gration Matovu kutoka Tanga. Kamisaa alikuwa Balozi B.J. Maggid, aliyekuwa Rais wa FAT, wakati mgeni rasmi alikuwa Rashid Mfaume Kawawa, Makamu wa Pili wa Rais.

Thursday, February 26, 2015
CHIDY BENZ AHUKUMIWA
Msanii hip hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' amehukumiwa miaka miwili kwenda jela.
Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam ambako kesi yake ya kukamatwa na madawa ya kulevya ilikuwa inasikilizwa.
Hukumu ilikuwa ni adhabu ya miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh 9,000,000 ambayo aliilipa baada ya watu wake kujitokeza na kukamilisha hilo na sasa Chid Benz.
Kesi yake hiyo iliyoendeshwa kwa wiki kadhaa, ilitokana na msanii huyo kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akiwa njiani kwenda mjini Mbeya kwa ajili ya shoo.
Chid Benz alikiri madawa aliyokamatwa nayo kwenye mfuko wa shati yalikuwa yake.
Sunday, February 22, 2015
BREAKING NEWSS , CHRISTOPHER ALEX AFARIKI DUNIA
PENALTI ILIYOIPA KIBURI SIMBA SC YAZIMIKA GHAFLA
Saturday, February 21, 2015
BALLOTELI AJIBU MAPIGO YA GERRALD
Bao pekee la mshambuliai mtukutu Mario Ballotel liliisaidia timu yake kuweza kuibuka na ushindi wa goli hilo moja dhidi ya wageni wao Besikitas katika round ya kwanza ya 32 bora Europa League, bao hilo lilipatikana mnamo dakika ya 85 kipindi cha pili kwa njia ya Penalt.
Licha ya bao hilo kupatikana Steven Gerrard amemuonya mshambuliaji huyo aliykipiga wakati huo akiwa na Inter Milan, Ac Milan, Manchester City na pia Liverpol kwasasa kuwa hakuonesha heshima kwa Captain wake Henderson kufanya uamuzi wa kumpokonya mpira na kupiga penalt maana alifanya kitu ambacho hakikuwa sahihi, na hayo yalionekana mara baada ya winga Jordan Ibe kufanyiwa faulo eneo la hatari.
Mshambuliaju huyo alimpokonya mpira Jordan Henderson mkononi huku akizinguana na Daniel Strurridge kabla hajaenda kupiga.
Captai mstaafu Steven Gerrard alisema
“Henderson ni kapteni na Ballotel alimuoneshea heshima isiyo sawa kumpokonya mpira, sharia ni sharia tu” Gerrard alisema na pia aliongezea kwa kumpongeza Ballotel kufunga hiyo penalt na kuipa ushindi Liverpool
lakini akisisitiza kusema sio vizuri kuwaona wachezaji wakibishana uwanjani na kumaliza akisema “Nadhani Henderson amekubaliana na hali vizuri”
BALOTELLI AJIBU MAPIGO YA GERRARD
Baada ya hapo awali nahodha wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard kusema kuwa kitendo cha mshambuliaji wa klabu hiyo Mario Balotelli kuchukua mpira kwa kiungo Jordan Henderson na kwenda kupiga penati ni utovu ni nidhamu,mshambuliaji huyo amejibu mapigo hayo ili kuondoa mzozo uliozagaa katika sehemu mbalimbali.
Balotelli amesema anamshukuru Henderson kwa kumpa nafasi ile na kufanikiwa kuleta ushindi muhimu kwa timu.
Liverpool iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Besiktas katika mechi iliyopigwa jana Anfield ikiwa ni mechi ya michuano ya europa ligi hatua ya mtoano huku goli hilo lililofungwa dakika ya 85 na Balotelli kwa mkwaju penati likizua utata ikionekana kuwa mchezaji huyo raia wa italia alimpokonya mpira Jordan Henderson ili akapige penati.
Hii imeshawahi kutokea katika klabu ya Everton walipokuwa wanacheza dhidi ya Westbromich January 19 mwaka huu katika uwanja wa Goodson Park ambapo Kevin Mirallas alimpokonya mpira Leighton Baines na na kwenda kupiga penati na matokeo yake akakosa.
Ushindi huu wa Liverpool unawapa nguvu ya kusonga mbele katika michuano hiyo wakiwa wanasubiria mechi ya marudiano itakayopigwa tarehe 26/2/2015 kule mjini Instanbul nchini Uturuki.
Aidha goli hilo la Balotelli ni la nne kuifungia klabu hiyo tangu asajiliwe msimu huu kwa ada ya Paundi milion 16 akitokea nchini Italia katika klabu ya AC Milan.