ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, October 8, 2013

BREAKING NEWSSSS, Henry Joseph azuiwa kuingia kambini

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Henry Joseph, amezuiwa kuingia kambini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuingilia mamlaka ya benchi la ufundi.

Mchezaji huyo ambaye amerudishwa tena msimu huu baada ya kutoka Norway alipokuwa anacheza soka la kulipwa,ameingia katika wakati mgumu huku kisa hicho kikikolezwa zaidi na mmoja wa kiongozi katika benchi la ufundi(jina linahifadhiwa ), ambaye amedai kuwa mchezaji huyo hapaswi kuingilia mamlaka ya benchi la ufundi.

Wakati huohuo, kiungo maridhawa wa Simba Jonas Mkude anatarajia kuanza mazoezi mepesi leo hii, Jonas ambaye jana hakufanya mazoezi na wenzake , leo atakuwepo katika fukwe za Bamba Beach katika kujiandaa na mechi dhidi ya Prison itakayopigwa siku ya jumamosi.

No comments:

Post a Comment