ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, October 10, 2013

Wanne tu kati ya wote waliosajiliwa hawapo kambini

Ikiwa siku chache baada ya kutolewa taarif a ya kuwa Simba SC baadhi ya wachezaji wake kuingia kambini, SPS imegundua kuwa ni wachezaji wane tu ambao hawapo kambini.
Wachezaji hao ni Ramadhan Chombo Redondo, Henry Joseph Shindika, Rashid Ismail Mkoko na Andrew Ntalla.

Ramadhan Chombo Redondo

Kiungo huyu maridhawa ambaye ni fundi haswa, amezuiwa kuingia kambini tangu jumatatu ya wiki hii.
Uchunguzi wa blog hii unaonesha kuwa, sababu kubwa iliyosababisha kuondolewa kambini ni nidhamu mbovu dhidi ya waalimu ndani na nje ya uwanja, SPS ilifika katika uwanja wa kinesi siku ya jumatatu na kushuhudia Redondo akiondoka kivyake huku wachezaji wengine wakipanda basi la wachezaji kuelekea Bamba beach ambapo kambi ya muda imewekwa hapo.
Katika hatua nyingine, kiungo huyu kuna uwezekano wa kurudishwa siku chache zijazo ingawa kocha mkuu amemwambia afanye mazoezi na timu B.


Henry Joseph Shindika

Baada ya swahiba wake Ramadhan kumkuta hayo, kiungo mkabaji ambae pia ni nahodha wa zamani wa Simba SC Henry Joseph naye amezuiwa kuingia kambini tangu siku ya jumatatu.

SPS ilivyofika uwanja wa kinesi ilimkuta Joseph akiendelea na mazoezi kama kawaida lakini la kusikitisha baada ya muda wa kuingia garini akazuiwa.

Baada ya kutokea hayo, timu yetu iliamua kufanya  uchunguzi wa kina na ndipo ilpopiga hodi kwa kocha msaidizi wa Simba SC Jamhuri Kihwelo Julio na kumuuliza kulikoni, Baada ya kuulizwa hivyo, Julio alijibu kuwa wachezaji wengi hawapendi mazoezi magumu kiasi cha kupelekea baadhi yao kusimamishwa, ila ni hali ya kawaida tuna imani kama benchi la ufundi watabadilika na kuja kuitetea Simba.

Kuhusu kumtoa mshambuliaji mwenye nguvu Bentram Mombeki, Julio alisema lengo la kumtoa lilikuwa asiweze kupewa kadi zaidi kwa kuwa tuna mechi ngumu tatu zilizofatana.

Rashid Ismail Mkoko

Kinda hili kutoka timu B, naye ameingia kwenye mkumbo baada ya kile kinachoitwa kushuka kwa kiwango chake, wakati yeye pia akiambiwa akafanye mazoezi na timu B yaani kule alipotoka mwanzo, swahiba wake kipenzi Edward Christopher yeye amejumuishwa kikosini na anaendelea na mazoezi kama kawaida.

Andrew Ntalla

Kipa huyu aliyesajiliwa wiki moja tu kabla ya kuja kwa kocha mpya Abdallah Kibaden ambaye amekuwa gumzo kwa kuonesha uwezo dhaifu na wa chini kabisa, ameomba ruhusa ya kwenda kumuuguza bibi yake mkoani kagera, wakati hayo yakiendelea SPS ilimkuta kipya mpya ambaye jina lake lilishindwa kupatikana haraka, akifanya mazoezi pamoja na Simba huku ikidaiwa kinda hilo jipya linatarajiwa kumwaga wino dirisha dogo la usajili, hii inatokana na uwezo wa hali ya juu anaoonesha kipa huyo mwenye umri chini ya miaka18.

No comments:

Post a Comment