ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, October 4, 2013

Chollo kuiongoza Simba leo dhodi ya Ruvu Shooting

Mchezaji aliyekosa takriban michezo miwili na Captain wa wekundu wa msimbazi Said Nassoro Chollo ,leo anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakachowavaa wanajeshi wa Ruvu Shooting ya mkoani pwani.

Hii itakuwa mechi yake ya kwanza baada ya kutoka kuwa majeruhi huku akikumbuka kikosi chake kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wanajeshi wengine wa JKT Ruvu.
Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua, itachezwa majira ya saa 10.00 jioni huku ikishuhudia baadhi ya wadau wakiiangalia LIVE katika televisheni ya TBC1

MUNGU IBARIKI SIMBA SC

No comments:

Post a Comment