ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, October 29, 2013

Kaseja ajifua na Simba ya Matola

Aliyekuwa kipa namba moja wa Simba Sc kabla ya kumaliza mkataba wake Juma Kaseja, ameendelea kujifua na Kikosi B cha Simba kinachofundishwa na nahodha wa Zamani wa timu hiyo Selemani Matola.

Juma Kaseja Juma ambaye siku chache zilizopita aliachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa kigezo cha Kukosa timu, ameonekana Hana wasiwasi wowote katika mazoezi hayo yanayoendelea katika shule ya msingi Mwenge .

Huku akiamua kuchukua jukumu la kuwanoa makipa wa timu B ya Simba,  Juma alionekana mchangamfu na yupo makini na mazoezi wakati wote.

Wakati Huohuo , Viungo washambuliaji wa timu ya Simba Ramadhan Chombo na Haruna Chanongo, wameendelea kufanya mazoezi katika kikosi hicho cha u20 ya timu ya Simba.

1 comment:

  1. bora kipa w2 tumrudshe maana yule jmaa aliebakia ni mlingoti tu hamna kitu kabisa

    ReplyDelete