ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 5, 2013

SIMBA YALAZIMISHWA SARE NA RUVU SHOOTING

Simba SC leo imeambulia pointi moja tu katika pointi tatu,baada ya kulazimishwa sare na Ruvu shooting.
Haikuwa kazi rahisi kwa Simba kwani vijana wa Ruvu walionekana moto kipindi chote cha mchezo wa leo,mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Ruvu shooting walikuwa mbele kwa goli moja walilofunga dakika ya 10 baada ya uzembe wa beki za kati za Simba.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi, hiuku mashambulizi yakiwa pande zote na ilikuwa dakika ya 69 pale mchezaji wa Ruvu Shooting alipomsukuma Mshambuliaji Bentram Mombeki katika eneo la hatari na ndipo mrundi Amissi Tambwe alipoweka kimiani mpira bila ajizi. Mpaka mpira unamalizika dakika ya 90, Ruvu Shooting 1-1 Simba,.

No comments:

Post a Comment