ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, November 12, 2013

Breaking Newssssssssss! Viwanja Sita vyapoteza hadhi ya kuchezewa Ligi kuu

Bodi ya ligi , imevifungia viwanja Sita vilivyokuwa vinachezewa ligi kuu Tanzania bara mpaka pale marekebisho stahiki yatakapofanywa.

Viwanja vilivyokumbwa na rungu hilo ni Kaitaba wa mjini Bukoba,Mkwakwani wa jijini Tanga,Sokoine wa jijini Mbeya,Amri Abeid wa jijini Arusha,Ally Hassan Mwinyi wa Tabora, na Jamhuri wa mkoani Dodoma.

Wakati Huohuo, michuano ya Kombe la Uhai linaloshirikisha timu za pili za ligi kuu Tanzania bara inaanza kutimua vumbi tarehe 17 ya mwezi huu.

No comments:

Post a Comment