ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, November 12, 2013

Dhaira kusuka ama kunyoa Simba Sc

Goli kipa namba mbili kwa sasa baada ya Abuu Hashim , Abel Dhaira anatarajiwa kuuzwa au kusitishiwa mkataba wake na Klabu ya Simba Sc siku chache zijazo.

Habari za uhakika ndani ya Klabu ya Simba sc, zinasema kuwa uamuzi huo unatokana na udhaifu alioonesha kipa huyo pia kanuni mpya za ligi kuu Tanzania bara zinazotaka wachezaji watatu tu wa kigeni ambao wanaweza kusajiliwa kwa timu mojawapo Kati ya zile  zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Wakati Hali ya kipa Dhaira ikiendelea kuwa na utata, goli kipa mwingine aliyesajiliwa kwa mbwembwe ili kuziba nafasi ya Juma Kaseja ambaye alimaliza mkataba wake Andrew Ntalla ameomba kuondoka katika Klabu hiyo baada ya kutoonesha Kiwango kisichoridhisha.

Ikionekana Kama ni Siri kwa Andrew Ntalla, blog hii inafahamu kuwa Ntalla anaondoka kwa sababu ya kuchoka kuzomewa na mashabiki wa Simba ingawa Baadhi ya Viongozi wa timu hiyo wanamkingia kifua!

No comments:

Post a Comment