ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, November 5, 2013

HUMUD, CHANONGO WAITOSA SIMBA





Wachezaji wawili wa timu ya Simba Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud wamekacha mazoezi yanayofanywa na Klabu Yao takriban  siku mbili baada ya kuruhusiwa kurejea Toka Simba B.

Humud na Chanongo, walipelekwa Simba B baada ya kufanya vibaya kwa dakika 45 katika mechi iliyowakutanisha dhidi ya watani wao wa Jadi .

Hali hiyo ilipelekea wachezaji hao kupelekwa timu B lakini ni Chanongo , Redondo na Henry Joseph ndio waliokuwa wanahudhuria mazoezi hayo Huku Henry na Redondo wakiwa washajiunga na wenzao.

Wakati Hali ya kambi ikiwa hivyo, timu hiyo kesho majira ya saa 10 inatarajiwa kucheza mechi ya mwisho katika raundi ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya watoto wa Ilala Ashanti Fc.

No comments:

Post a Comment