ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, November 5, 2013

Simba yaapa kufa na Ashanti kesho








Timu ya soka ya Simba Sc kesho inaingia katika raundi ya mwisho ya mzunguko wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa na deni la ushindi dhidi ya mashabiki wake ambao wamekosa amani na timu hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiongea na blog hii, wamesema kuwa wanatambua kuwa wana deni kubwa kwa mashabiki wao ingawa mpira ni mchezo wa makosa watajitahidi kadri wawezavyo ili waweze kuibuka na ushindi.

Timu hiyo iliyokosa muelekeo kwa takriban mechi tano zilizopita, imeweka kambi katika fukwe za Bamba Beach nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam kesho itashuka dimbani bila kuwepo kwa nahodha wake Said Nassoro Chollo aliyekuwa majeruhi!

No comments:

Post a Comment