ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, November 3, 2013

Kibaden akalia kuti kavu Simba Sc

Kocha wa Simba Abdallah Kibaden , yupo katika wakati mgumu kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo .

Hii inatokana na kikao kilichokaa siku chache zilizopita cha viongozi wa Simba kutaka kumtupia virago kwa kutoridhishwa na mwenendo wa Klabu.
Katika mechi tano zilizopita, Kikosi hicho cha mtaa wa Msimbazi, kimejinyakulia points nne tu Hali inayozidisha ugumu wa kunyakua Taji la ligi kuu Tanzania bara!

Katika hatua nyingine, habari za ndani ya Klabu zinasema, Uongozi wa Simba unafanya mazungumzo na kocha wa Zamani wa Uganda Bob Williamson ili aweze kuichukua Simba mzunguko wa pili unaoanza Januari!

No comments:

Post a Comment