ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, November 6, 2013

UWANJA WA TAIFA HATARINI KUHARIBIKA

Hali ya uwanja wa Taifa wa Tanzania maarufu Kama Benjamin Mkapa National Stadium ni mbaya kiasi cha kupelekea watu kutoamini Kama ndio huo.

Blog hii ilifika katika uwanja wa taifa katika kushuhudia mechi Kati ya Simba na Ashanti na kukuta uchafu mwingi vyooni, Hali inayoonekana kuwa haujasafishwa kwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Katika upande wa pitch ( Nyasi) , Blog hii ilishuhudia nyasi dhaifu na zilizochoka katika uwanja huo, Kana kwamba uwanja huo umejengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Ikumbukwe kuwa, kila mechi inayochezwa katika uwanja huo, mamilioni ya pesa hukatwa kwa ajili ya kufidia gharama za umeme, usafi nk katika uwanja huo.

No comments:

Post a Comment