ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, November 8, 2013

WANACHAMA WALIOKAMATWA SIMBA WAACHIWA KWA DHAMANA YA BILIONI MOJA

Wanachama wa Klabu ya Simba ya jijini Dar Es Salaam Leo wameachiwa hurry kwa dhamana ya Mali isiyohamishika.

Awali ya hapo, mahakama iliwaambia watuhumiwa hao 11 kuwa kila mmoja apeleke pesa kiasi cha Sh 900000/= za Tanzania pamoja na mdhamini mwenye Mali isiyohamishika, Hali hiyo ilipelekea wanachama hao kutojua la kufanya Huku wakisema kuwa mdhamini mwenye Mali isiyohamishika ni ngumu kuwapata, baada ya majidiliano ya Muda mrefu, Klabu ya Simba ilihamua kutoa moja ya hati ya majengo yake inayomiliki mtaa wa Msimbazi, yenye gharama ya zaidi Billioni moja Hali iliyopelekea kuachiwa huru kwa Muda huku kesi Yao ya Msingi ikiendelea!

Wiki iliyopita , Baadhi ya wanachama wa Simba Sc walianzisha vurugu kiasi cha kupelekea kuvunjwa kwa Baadhi ya viti uwanja wa taifa kwa kile kilichodaiwa ni uonevu wa wazi wa Refarii baada ya kutoa penati yenye utata dhidi ya Simba katika pambano la ligi kuu ya soka Tanzania bara!

No comments:

Post a Comment