ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, March 9, 2014

BREAKING NEWSSS: DIDA HATI HATI KUFUNGIWA NA CAF

Kipa namba moja wa washiriki wa mwaka huu katika michuano ya klabu bingwa Afrika Deogratius Munishi maarufu kama Dida, ameingia rasmi katika mtego wa maisha yake ya soka baada ya camera za uwanjani zikimuonesha akifanya mambo yanayoashiria ushirikina katika goli lake.

Dida ambaye jana alidaka kwa kiwango cha juu, amerudia kitendo aslichofanya katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo Yanga walishinda goli 1-0, hali iliyopelekea kamati maalum ya CAF kukaa siku chache zijazo kujadili tukio hilo lote.

Kama kipa huyo atapatikana na hatia, basi adhabu yake inaweza kufungiwa michuano ya CAF au kupigwa faini kwa matendo yake hayo.

Wakati huo huo hali ya kambi ya timu ya Yanga ni mvurugano baada ya kufurumushwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

Habari za ndani ambazo SPS imezipata, inasema kuwa viongozi wameumia sana na matokeo hayo na wanatarajiwa kufanya kikao cha siri watakapofika jijini Dar es salaam!

No comments:

Post a Comment