ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, March 10, 2014

RAGE HANA CHA KUJIVUNIA SIMBA SC, NI WAKATI WA KUJIWAJIBISHA YEYE MWENYEWE

Wakati Ismail Aden Rage anaingia madarakani, hakika kila mdau au mwanachama wa Simba alitegemea mazuri chini ya uongoz wake.

Mbwembwe alizoingia nazo kiasi cha kuwafukuza baadhi ya wachezaji wa Simba pale alipoingia tu kwa kigezo cha eti wachezaji hao ni mamluki kilitosha kabisa kuthibitisha kuwa Rage hakuwa na lengo zuri sana kwa timu hii ya mitaa ya msimbazi.

Sio wachezaji tu kwani hata makocha yeye alitimua sifikiri ilikuwa kwa malengo mazuri kwani timu iliyumba na inaendelaea kuyumba mpaka sasa.
Wakati anaingia  mheshimiwa huyu aliikuta Simba SC ikiwa ni mabingwa wa Tanzania tena ni timu inayotikisa nchi nzima ila kwa sasa sio Simba tena kwani sasa hivi kufungwa na Jkt mgambo au Jkt ruvu ni kitu cha kawaida.

Ingawa kiumbe hiki kinatumia akii nyingi kwa kuwazuga wanachama na mashabiki kwa kigezo cha udhaifu wa katiba na kigezo cha wanachama kutotaka kuijua wala kuisoma ile katiba, ni vyema Rage atambue kuwa walio wengi ya wanachama wamemchoka.

Hakuna asiyefahamu kuwa aliiondoka na leja nyumbani kwake, hakuna asiyefahamu yanayoendelea pale nyuma ya sekondari ya kisutu.

Kwa kifupi Rage inabidi ajiwajibishe kama kweli nyeye yupo kwa ajili ya Simba cSC, kinyume na hapo atakuwa anatudanganya na atakuwa mmoja wa mamluki ndani ya Simba SC.

Simba ni kwa ajili yetu sote!

No comments:

Post a Comment