ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, March 13, 2014

WANACHAMA SIMBA WAPINGA AJENDA MOJA SIKU YA JUMAPILI

Baadhi ya wanachama wa Simba SC leo wamejitokeza katika ukumbi wa idara ya habari na maelezo kupinga kabisa uwepo wa ajenda moja siku ya jumapili.

Wakiongea mbele ya waandishi wa habari, mwanachama anayetambulika kwa jina la Bi Hindu,amesema si sahihi kwa mwenyekiti kuitisha mkutano ukiwa na lengo la ajenda moja na kufanya hivyo kunaweza kutokea vurugu siku ya jumapili.


Wakati huo huo, katibu mkuu wa Simba SC bw Ezekiel Kamwaga amesema kuwa marekebisho ya katiba yatafanywa katika vipengele ishirini vilivyopo katika katiba hiyo,

Huku hali ikiendelea hivyo upande wa pili yaani Yanga SC , umeapa kuandamana nchi Zima kama manispaa ya ilala haitawaongezea eneo kwa ajili ya kutengeneza uwanja wao.

No comments:

Post a Comment