ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, June 5, 2014

BOBAN; NIKO TAYARI KURUDI SIMBA SC

Aliyekuwa kiungo wa Simba Sc ambaye alishindwa kuongezewa mkataba wake na kuamua kwenda Coastal Union Haruna Moshi Shaaban maarufu kama Boban, amesema kuwa yiko tayari  kurufi Simba Sc muda wowote kama itahitajika.

Boban ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Simba Sc, ametamka maneno hayo akiongea moja kwa moja na SPS.

Akiwa mwenye tabasamu, kiungo huyo mtukutu na ambaye ni fundi wa soka amesema kuwa atarudi Simba Sc kufanya kazi.

Wakati huo huo, mgombea wa nafasi ya umakamo wa urais wa Simba Sc ametamka kuwa kiungo huyo atakuwa wa kwanza kumsajili kama ataingia madatakani.
Mgombea huyo ambaye aliomba kutotajwa jina lake, amesema ahadi hiyo ataikamilisha mara moja punde tu atakapoingia madarakani.

No comments:

Post a Comment