Shirikisho la soka nchini Tanzania limepatwa na aibu ya mwaka baada ya basi lake kukamatwa leo hii.
Kampuni ya kutengeneza tiketi yenye makazi yake nchi kenya,limezuia basi hilo baada ya TFF kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 140 ikiwa kama gharama za kutengenezea tiketi za TFF,. Akiongea na waandishi wa habari leo hii, Afisa habari wa shirikisho la soka nchini Boniface Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo." Ni kweli wamezuia basi,ila tunafanya mchakato ili tuweze kuliondoa mikononi mwao " Wambura aliongeza.
Ikumbukwe kuwa,kwa kilaechi inayochezwa nchini, lazima TFF wakate asilimia kadhaa ya kiasi kinachopatikana kikiwa kama gharama za malipo ya tiketi.
No comments:
Post a Comment