Kiungo mshambuliaji wa Simba SC Uhuru Selemani,amefurahishwa na ujio wa kocha wa sasa Patrick Phiri kisha kutamka maneno machache " kazi imeanza".
Mchezaji huyo ambaye hakuwa chaguo wa kocha aliyefungishiwa virago Zdravko Logarusic, amesema kuwa atajituma sana ili authibitishie umma kuwa Loga alikuwa anakosea.
Katika mazoezi yaliyofanyika leo katika uwanja wa Boko Veteran, Uhuru alionesha uwezo wa hali ya juu kiasi cha baadhi ya mashabiki kumpigia makofi kuonesha kuukubali uwezo wake.
Wakati huo huo, kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kuondoka kesho saa 10.00 jioni na boti badala ya saa 2.00 asubuh.
Mabadiliko hayo yamefanywa ili wachezaji wote wajiandae vizuri kwa safari hiyo inayotarajiwa kuwa yenye neema baada ya miaka kadhaa ya kukosa ubingwa kwa klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment