ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, August 18, 2014

AWADH JUMA,BENTRAM MOMBEKI NI MTEGO KATIKA SIMBA YA PHIRI

Wiki hii kumekuwa na taarifa zinazochanganya kuhusu wachezaji wawili wa Simba SC, wachezaji hao ni Awadh Juma na Bentram Mombeki.


AWADH JUMA
Ni mchezaji wa Simba SC ambaye aliingia Simba SC na kuonesha uwezo wa hali ya juu,ndiye alikuwa nyota wa mchezo wakati Simba SC inaiangamiza Yanga goli 3-1, kwa maana hiyo ni mchezaji anayejua.
Kwa siku kadhaa mchezaji huyu kuna taarifa kuwa anapelekwa kwa mkopo katika timu ya Stand United, ingawa mpango huu ulikuwa tangu alipokuwa kocha Zdravko Logarusic lakini mpaka sasa mpango huo bado upo ingawa kuna kocha mpya Patrick Phiri, na hakuwahi kumuona Awadh akicheza, je ni nani hasa mwenye uwezo wa kumtoa Awadh Juma Kwa mkopo kutoka Simba SC? muda utaongea


BENTRAM MOMBEKI
Huyu ni staa wa Simba Sc ambaye alifanya makubwa wakati wa kocha Abdallah King Kibaden, bahati mbaya hakuwa na wakati mzuri alipokuwa kocha Zdravko Logarusic,, ingawa ni mchezaji mzuri sana lakini aliwekwa kati ya wale wachezaji wasiokuwa na nafasi ndani ya Simba SC, siku kadhaa zilizopita imeripotiwa kuwa Mombeki anahitajika kurudi ndani ya Simba SC, Je Phiri alimuona wapi Bentram,,huwezi kujua ila muda utaongea.

1 comment: