Mchezaji Kiggy Makassy amerejea nchini toka India alipokuwa amepelekwa kufanya matibabu ya goti lake. Kiggy amerejea na kusema kuwa ataanza mazoezi rasmi muda si mrefu ili aweze kupata nafasi ya kucheza katika klabu, akiongea kwa furaha na kujiamini, alisema amefurahishwa na hatua ya klabu yake kumpeleka India ingawa alichelewa katika matibabu hayo, pia amesema matibabu yalikwenda vizuri sana.
No comments:
Post a Comment