ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Thursday, February 5, 2015

AZAM TV NA KIFO CHA SOKA LA TANZANIA!


KWA HILI LA AZAM TV MMH!.                         Jumapili iliyopita Kituo cha Televisheni cha AZAM TV kiliingia mkataba wa miaka miwili na nusu na Klabu zinazoshiriki ligi kuu Uganda pamoja na Shirikisho la soka Uganda (FUFA).Kwa makubaliano yaliyofikiwa siku hiyo hatimaye sasa kila klabu inayoshiriki Ligi Kuu Uganda itaambulia Tshs 28.5 Millioni sawa na Dola 16'363.Fedha hizi zitakuwa ni kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi utakaoanza mwezi Februari tarehe 13.Kwa maana kwamba kituo hicho kitaonesha mechi zote za mzunguko wa pili za Ligi Kuu Uganda na hivyo kufanya Ligi Kuu ya Uganda kujulikana kwa jina la "Azam Uganda Premier League".Azam TV imewekeza Tshs 3.8 bilioni za kitanzania kudhamini ligi hiyo.Licha ya kuwapongeza Azam kwa kujitangaza wao na biashara yao lakini tunaamini hawakufanya jambo la uzalendo kwa soka la Tanzania kutokana na ukweli halisi kuwa soka la ukanda huu wa Afrika Mashariki Tanzania imeendelea kudorora vibaya sana kulinganisha na majirani Kenya,Uganda,Rwanda,Zambia,Congo nkAzam sasa wanataka kudhamini ligi kuu ya DRC na Rwanda na iwapo itadhamini Ligi hizo zote kwa kima hicho hicho kama ilivyofanya ktk Ligi Kuu ya Uganda basi maana yake itakuwa imewekeza zaidi ya UsD 6.75 milioni sawa na 11.4 Bilioni.Na fedha hizo ni bila ya hizi ilizowekeza katika Ligi Kuu Tanzania Bara.Kwa hakika habari hii hatudhani kama ina nia nzuri na ya kizalendo ya kuendeleza mpira wa Tanzania kwa ujumla kwa kuwa binafsi tulidhani kuwa AZAM TV wangeweza kuboresha Ligi ya nyumbani Tanzania Bara kwa mfano,licha ya kutoa Tshs 100 Milioni kwa mwaka kwa kila klabu inayoshiriki Ligi Kuu hapa Bara ingeweza kuongeza fefha hizo ilizotoa kwa vilabu vya Uganda (28.5 Milioni) kwa kila klabu na tunaamini kama ingetoa pia kwa vilabu vya Congo DR na Rwanda kiasi kama hicho basi ni sawa na kusema kuwa kila Klabu inayoshiriki Ligi Kuu Bara ingenyakua fedha Tshs 185.5 milioni Kwa kila mwaka wa Ligi.Fedha hizi bila shaka yoyote zingesaidia harakati za kusogeza mbele mpira wa Tanzania na sio mpira wa Uganda,Congo DR ama Rwanda ambapo bidhaa za Azam hazina soko kubwa kama hapa Tanzania.Kwa kufanya hivyo Azam TV ingekuwa imeleta mapinduzi makubwa ya soka la Tanzania na hii ingekuwa njia rahisi za kuepuka rushwa na magumashi kadhaa ndani ya soka letu lenye kiza.Leo Azam wanawekeza Uganda,sina hakika lengo hasa kama watanzania ambao ndio wanunuzi wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa na Azama Group of Companies,tutapata maslahi yoyote.Tunaamini kuwa na udhamini mzito wa kuonesha ligi yetu Tanzania basi tungeweza kuitangaza haraka nchi kwa ujumla pamoja na wachezaji wetu kuwa na soko la haraka kuliko ilivyo sasa.Leo Azam wanaingia ktk mkataba wenye kila kiashiria chenye utofauti na wanaoonesha mpira wa Uganda kwa sasa (Super Sport).Ni jukumu kubwa la Azam TV kutupia macho soka la nyumbani.Inasikitisha kuona Azam inaenda Uganda kuwekeza mabilioni ktk Ligi yao huku ikiwa inanyemelea kujitangaza huko Congo DR na Rwanda huku ikisahau hata upande mmoja wa nchi (Zanzibar) ambapo kutokana na kukosa udhamini wa uhakika wa  Ligi ZFA wamekuwa wakitegemea udhamini mdogo kabisa wa Tshs 8 milioni kwa kudhamini timu 12 zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.Udhamini huo mdogo wa Grand Malt unatolewa kwa awamu 2 na kila awamu inatoka Tshs 4 milioni.Kiukweli udhamini huo haukidhi kabisa hata mahitaji ya ZFA.Lakini leo tunashuhudia Azam TV wakitoa mamilioni kutangaza Ligi za waganda,hata Wacongo na Warwanda .Tunaamini Ligi Kuu yetu utaangaliwa kwa jicho kali sana kuhakikisha tunaondoa mashaka yoyote ya viashiria vya dhulma,mizengwe,chuki,fitina na upangwaji matokeo iwapo tu tutawapata wawekezaji kama hao Azam TV watakaoamua kuwekeza nyumbani na sio huko wanapojaribu kuwekeza sasa hivi.Tunasema hivyo kwa kuwa tunaamini fedha zote hizo ni sehemu ya  fedha zetu  watanzania ambao tumekuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa bora za Azam Group of Companies ambao wanamiliki Azam TV pia.

No comments:

Post a Comment