ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 19, 2013

DAKIKA 90 ZA HESHIMA MSIMBAZI

Naaam,tunaweza kusema kuwa ni dakika 90 za heshima msimbazi leo, pale timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam itakapokuwa inawavaa watani wao wa jadi Yanga SC,katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa taifa.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na timu zote mbili, itachezeshwa na refa Israel Nkongo ambae ana beji ya FIFA.
Simba yenye wachezaji nyota ambao waliiwezesha timu hiyo kunyakua kombe la Banc ABC super 8, leo inatarajiwa kuwaonesha Yanga kuwa wao walistahili kuwa mabingwa wa michuano hiyo iliyofanyika msimu uliopita.

Wakati huohuo, timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, leo inatarajiwa kuchekelea kwa kushuhudia urejeo wa beki yake ya kushoto, Idrissa Rashid, maarufu Baba Ubaya.

No comments:

Post a Comment