ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 19, 2013

Patrick Leiwig kuishuhudia Simba ikimenyana na Yanga kesho Taifa

Kocha aliyetimuliwa Simba Sc mfaransa Patrick Leiwig, kesho anatarajia kuwa mmoja wa watazamaji katika uwanja wa Taifa, kuishuhudia Simba ikimenyana na Yanga katika muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Leiwig ambaye anasifika kwa kuwaamini vijana kufanya kazi, aliwasili jana na kufikia katika hotel ya Saphirre jijini Dar es Salaam huku ikidaiwa kuwa lengo lake kuu la kufika Tanzania ni kudai baadhi ya pesa zake anazoidai klabu ya Simba.

Baadhi ya wachezaji makinda waliokuwa wakiaminiwa na mfaransa huyo ni Abdallah Seseme, Willium Lucian Gallas , Ramadhani Singano na Said Ndemla

Ikumbukwe kuwa, mara ya mwisho kocha huyo aliiongoza Simba kupigwa kipigo cha magoli 2-0, dhidi ya Yanga, katika mchezo wa mwisho wa kufunga msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment