ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, October 22, 2013

Humud, Chanongo watoswa Simba

Siku moja baada ya kuonesha Kiwango kibovu katika mechi ya watani wa Jadi, viungo wawili wa timu ya Simba Abdulhalim Humud na Haruna Chanongo, wameachwa katika msafara ulioelekea Tanga siku ya Jana kwa Madai ya udhaifu wa viwango vyao.

Kocha mkuu Abdallah Kibaden, amesema viwango walivyoonesha nyota hao ni vya Hali ya chini, hivyo hawana budi kwenda kuviimarisha katika kikosi cha pili cha Simba kinachonolewa na Nahodha wa zamani wa Simba Sc, Selemani Matola ( Veron)

Timu ya Simba, Jana majira ya Asubuhi, waliondoka jijini Dar Es Salaam kuelekea mkoani Tanga, watakapocheza mechi ya ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union hapo kesho.

No comments:

Post a Comment