ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Friday, October 25, 2013

Dhaira kamili kuwazuia Azam jumapili

Goli kipa namba moja wa Simba Sc Abel Dhaira, yuko vizuri kukaa langono siku ya jumapili kama kocha Abdallah Kibaden atampanga.
Kipa huyo raia wa Uganda ambaye alikuwa majeruhi, aliumia baada ya kugongana na nyota wa zamani wa Simba anayekipiga Coastal Union siku ya jumatano katika mechi ya muendelezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Wakati Dhaira akitarajia kurudi dimbani Jumapili, kiungo cha pembeni cha Simba Sc Ibrahim Twaha Messi, naye anatarajia kurejea baada ya kuwa nje kwa takriban wiki tatu.
Twaha alianza mazoezi siku ya jumanne tayari kuwavaa wana lambalamba wa Azam FC katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa timu hizo.

No comments:

Post a Comment