ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 26, 2013

Haya ya Saleh Ally na Ismail Aden Rage yanahitaji majibu kutoka kwao

Jana katika pitapita zangu za kuangalia kwenye baadhi ya blog nilifanikiwa kuona kitu cha ajabu kama si cha kawaida katika blog ya Saleh Ally.

Blog hiyo inayoitwa www.salehjembe.blogspot.com ilikuwa na moja ya habari iliyoandikwa kuwa RAGE ,SUALA LA OKWI HALIHITAJI UCHUNGUZI NA HAUTALIKWEPA, binafsi nilivutiwa sana na habari hii.
Ndani ya habari hii, Saleh alimzungumzia sana mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Afen Rage toka alipoichukua Simba mpaka timu yetu ilipofikia, kulikuwa na vipengele vingi sana ndani ya habari hiyo ambavyo vingine nilishawahi kuviona na vingine bado sijaviona.

Kiukweli ilinihuzunisha sana pale nilipoona kuwa hata Rage huwa ANANG'ANG'ANIA TIKETI ILI APATE 'PASU',sijaweza kukikubali hiki kipande wala kukitaa ila baada ya kukisoma kwa makini nilikumbuka siku moja ndani ya msimu huu timu yangu ya Simba ilipokuwa inacheza mechi ya kirafiki katika uwanja wa kinesi dhidi ya timu iliyokuwa inafundishwa na nahodha wa zamzni wa Yanga Shadrack Nsajigwa kuwa makamo mwenyekiti wa Simba aliwaibia mapato timu ya lipuli, na kauli hii ilithibitishwa na kiongozi mmojawapo wa timu hiyo ya Iringa.

Suala hili la Rage lililoibuliwa na ndugu Saleh ni zito sana na sio jepesi kama watu wanavyofikiri, kila nikikumbuka jinsi mapato ya Simba yanavyopatikana na mgao unavyokuwa napata mashaka sana jinsi uthabiti na umakini wa uongozi wetu, siwezi kuulaumu uongozi peke yake kwani hata TFF katika tuhuma hii wanaweza kuingia hapa.

Ila imefikia hatua Mwenyekiti wetu atuambie ukweli hadharani kuhusu hili au Bw Saleh Ally atuthibitishie ili kuokoa soka letu, kwa kuwa watu wanaumia,wnakufa kwa ajili ya timu zao na pasiwepo mtu mmoja anayeonekana ana maslahi binafsi kati ya Saleh na Rage ili waweze kufanya mambo yao pasipo kuangalia thamani ya klabu yetu .

No comments:

Post a Comment