ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, October 23, 2013

SIMBA KUREJEA DAR LEO

Timu ya soka ya Simba Sc, inatarajia kuwasili Dar es salaam leo, ikitokea jijini Tanga ilipokuwa katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union.

Timu hiyo ya mtaa wa msimbazi, jana ilikuwa na kibarua kizito dhidi ya watoto hao wa Tanga,kiasi cha kulazimishwa sare ya 0-0 , na kuambulia point moja tu.

wakati huo huo, hali ya kipa Abel Dhaira ambaye alishindwa kumalizia mechi siku ya jana na kumpisha kipa kinda Abuu Hashim inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment