ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Monday, October 7, 2013

FANYA KAZI YAKO IPASAVYO KIBADEN KWA MANUFAA YA SIMBA NA KIBARUA CHAKO

Ukinambia nichague kocha bora wa muda wote wa Simba, hakika mara moja nitamtaja kocha wa sasa Abdallah Kibaden, hii inatokana na rekodi yake safi aliyoiweka alipoifikisha Simba fainali ya kombe la CAF.

Hakika anastahili pongezi sana tena sana, Simba SC kwa sasa imeamua kumrudisha kocha mzalendo
baada ya kumtosa kocha toka ufaransa Patrick Leiwig kwa madai' hashauriki', sio mbaya sana kwa kuwa makocha wanaajiriwa lengo ni kupata matokeo bora uwanjani.

Katika msimu wa ligi kuu Tanzania bara, King kibaden ameiongoza Simba katika michezo saba, miwili ugenini na mitano nyumbani(uwanja wa taifa), mechi za ugenini ni dhidi ya Rhino ya Tabora 2-2, dhidi ya Jkt Oljoro ya Arusha 1-0, wakati mechi za taifa ni dhidi ya jkt mgambo 6-0,Mtibwa sugar 2-0,Mbeya City 2-2, Jkt Ruvu 2-0, Ruvu Shooting 1-1, kwa ujumla matokeo si mabaya kabisa kwa kuwa timu inaongoza ligi kwa idadi ya point 15 ukilinganisha na timu nyingine.

Sitaki na sitapenda kuzungumzia mechi za Tabora na Arusha lakini nitapenda nizungumzie mechi zilizopigwa taifa kwani zote nimeziona. Wahenga walisema msema kweli ni mpenzi wa kila mtu name nataka nichambue mechi zilizopigwa taifa.

Hakika mechi ambayo angalau timu ilicheza vizuri ni moja tu dhidi ya Mbeya City, nyingine zote ingawa tulishinda mpira ulikuwa si wa kuvutia, mbaya zaidi timu haina muunganiko wa kiuchezaji, wachezaji wanacheza namba ambazo hawajazizoea.

Mfano katika mechi tatu za mwisho, Amry Kiemba  alitumika kama namba saba , sijajua kwanini anachezeshwa namba hii wakati kiuhalisia Kiemba ni namba nane au kumi, udhaifu kama huu ndiyo unapelekea timu icheze hovyo, sio huyu tu angalia hata nafasi ngumu anayocheza Henry Joseph kwake, sikatai kwamba kocha ana maamuzi yake, ila mpira unachezwa hadharani na kila kitu kinajionesha, .

Siwezi kukubali kuwa kocha anaingiliwa katika kazi yake ila kama ni kweli basi anapotezwa, kwanini anapotezwa??? Ni kwa sababu hao wanaofanya hivyo baadae wanaweza kumgeuka na kumleta mwingine, muda umefika wa Kibaden kuthubutu kufanya kazi yake kwa usahihi bila kujali chochote, tunamuamini sana na muda bado upo.

Fanya kazi mzee ili watu waione kwani wewe ndiye kocha tunayekuamini kwa sasa,kinyume na hapo thamani ya ukocha itashuka pasipo wewe mwenyewe kutarajia.
 

No comments:

Post a Comment