ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, October 22, 2013

Tambwe aahidi magoli zaidi dhidi ya Coastal hapo kesho

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayechezea Klabu ya Simba ya Tanzania  Amissi  Tambwe, amesema atahakikisha anaiangamiza Coastal Union katika mchezo utakaopigwa kesho katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Akiongea na blog hii, mfungaji huyo bora wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, na ligi kuu ya Burundi amesema kuwa ligi ni ngumu sana ingawa timu yake inajitahidi kucheza vizuri zaidi ili iweze kuongoza ligi kabla ya mzunguko wa kwanza haujaisha na hayimaye kuchukua Ubingwa unaosubiriwa kwa hamu na wana Msimbazi.
Tambwe ambaye alionesha Kiwango safi katika mechi ya juzi , Ndiye aliyetoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Mshambuliaji wake Pacha, Bentram Mombeki katika mchezo ulioisha kwa sare ya goli 3-3, .

No comments:

Post a Comment