ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 19, 2013

KIEMBA YUKO VIZURI KUWAHENYESHA YANGA KESHO

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Amry Kiemba, yuko katika ari ya hali ya juu katika kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga SC.

Kiemba ambaye ni mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania bara kwa upande wa waandishi wa habari, anatarajia kuwaongoza wachezaji wenzake wa Simba ili kufanikisha azma yao ya kuibuka na alama zote tatu hapo kesho majira ya saa10.00 jioni.

Ikumbukwe kuwa, vijana hao wa msimbazi mpaka sasa hawajapoteza mechi yoyote ile ya ligi kuu tangu msimu huu mpya kuanza, hali inayopelekea mchezo wa kesho kuwa mgumu kuliko unavyotarajiwa na pande zote mbili.

No comments:

Post a Comment