ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Saturday, October 19, 2013

SIMBA YAAPA KUIUA YANGA KESHO

Timu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imeapa kuwa itaiangamiza timu ya Yanga kesho katika muendelezo wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Simba Sc, inayofundishwa na kocha mzawa Abdallah Kibaden, imejichimbia nje ya jiji la Dar ili kujiweka vizuri na mchezo huo unaotarajiwa kuvuta hisia za mamilioni ya Watanzania.

Katika michezo mitatu ya mwisho dhidi ya Yanga, timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi, imefanikiwa kuondoka na idadi ya magoli sita dhidi ya matatu ya watani wao hao ambao nao wanapewa nafasi ya kushinda mechi hiyo ya kesho.

No comments:

Post a Comment