ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, October 15, 2013

SIMBA YAZIDI KUIVUTIA KASI YANGA KUELEKEA OCT 20

Timu ya soka  ya Simba Sc ya jijini Dar es Salaam,leo imeendelea kuivutia kasi timu ya Yanga katika ufukwe wa Bamba beach,kuelekea katika mtanange wao utakaopigwa siku ya jumapili ya wiki hii.

Katika mazoezi yaliyofanyika leo, vijana walicheza kwa kasi ya hali ya juu na spidi ya ajabu,huku kila mchezaji akionesha nia ya kutaka kupewa nafasi katika mechi hiyo kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wakati huo huo, Kocha wa Simba SC, Abdallah Kibaden ameahidi timu itacheza soka safi na la hali ya juu, ili kuidhinisha ubora wa timu yake ambayo inasukwa na wachezaji wengi wapya.

No comments:

Post a Comment