ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Sunday, December 8, 2013

LUGARUSIC ; NATAKA KIKOSI KIDOGO

Kocha Mkuu wa Simba, Zravko Logarusic amesema hana nia mbaya na wachezaji atakaowaacha.

Badala yake anataka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mechi 13 zilizobaki za ligi na nyingi za mashindano.


“Tuna muda mchache sana na tunahitaji wachezaji wa aina fulani, hivyo sina ugomvi wala matatizo na nitakaowaacha.
“Wanatakiwa kuelewa tunafanya nini na ukichaguliwa maana yake umeonyesha uwezo,” alisema.

Kocha huyo ameamua kupunguza kikosi chake na kubakiza wachezaji wachache watakaowania namba kwa ushindani na kuisaidia Simba kurudisha hadhi yake.
Logarusic raia wa Croatia amechukua nafasi ya Abdallah Kibadeni ambaye sasa ametua Ashanti United.

No comments:

Post a Comment