ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Wednesday, December 4, 2013

MATOLA AANZA KAZI RASMI SIMBA

Baada ya mvutano wa hapa na pale, hatimaye kiungo Selemani Matola ameanza kazi ya kocha msaidizi chini ya Kocha Zradkov Logarusic.

Awali ilionekana Logarusic kukerwa na kuchelewa kwa Matola, lakini baadaye kukawa na taarifa kocha huyo wa vijana wa Simba alikuwa akisubiri ajadili mkataba wake mpya kama kocha msaidizi.

Lakini leo Matola ameungana na Logarusic na kuanza kupiga job kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam.

Taarifa zimesema tayari Matola amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba chini ya kamati ya utendaji na utampa mkataba mpya ambao umeboreshwa.

Matola ni kati ya makocha vijana wenye uwezo mkubwa na amekuwa akipigiwa chepuo kupewa timu kubwa.

Iliwahi kuelezwa angekuwa msaidizi wa Abdallah Kibadeni, lakini baadaye Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, beki wa zamani wa Simba, akaongezewa miezi sita kuendelea kuinoa timu hiyo.


Kibadeni na Julio wameondolewa Simba na nafasi zao sasa zitarithiwa na Logarusic raia wa Croatia na Matola ‘raia’ wa Kigoma.

No comments:

Post a Comment