ASASH GENERAL TRADERS

ASASH GENERAL TRADERS

Tuesday, December 17, 2013

RAGE ASEMA PESA ZA OKWI LAZIMA ZITUE SIMBA

Mwenyekiti wa timu ya Simba Sc Leo amekata mizizi wa fitna baada ya kuthibitisha kuwa Okwi ni mali ya Etoile na Simba Sc inaidai Etoile pesa hizo.

Akiongea na wanachama wa Klabu ya Simba katika makao makuu ya Klabu Msimbazi jijini Dar es Salaam, Rage alisema kwa hakika amesikitishwa na hatua walioifanya Yanga dhidi ya Okwi huku akitamka wazi kuna wasaliti ndani ya Klabu ya Simba wanaofanya kazi kwa manufaa ya Yanga.

Ikumbukwe kuwa Kauli hii ya Rage ni Kama marudio ya Kauli ya aliyekuwa kocha wa Simba Sc Milovan Cirkovic .

Ismail Aden Rage ambaye alisimamishwa na kamati ya utendaji ya Simba Sc, amesema kuwa hana Imani na kamati hiyo Huku akithibitisha uwepo wa mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji Bw Michael Wambura.

Wakati huo huo , Rage alionesha barua iliyotumwa na FIFA kwenda Klabu ya Simba ambayo iliitaka Simba ilipe kiasi cha Dola 5900 ili kesi waliyoipeleka Fifa isikilizwe ,.

Akiongea kwa uchungu Huku machozi yakimtoka , Bw Rage amesema kuwa barua ilifika Tangu tarehe 6 Dec lakini hakuna mjumbe yeyote wa kamati ya utendaji ambaye aliithubutu kuifanyia kazi kwa kuwa Muda uliopangwa na FIFA ulikuwa unaisha Leo Huku wajumbe hao wakitambua kuwa yeye hayupo.

Katika hatua nyingine, Rage amesema kuwa aliwataarifu wajumbe wa kamati ya utendaji wafike saa 9.00 alasiri kwenye mkutano huo Huku akishangaa kwanini hakuna mjumbe Hata mmoja aliyefika!

No comments:

Post a Comment